Ubao wa matokeo katika mchezo uliozikutanisha timu za Yanga na Mtibwa katika Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ukionesha timu hizo kuwa 0-0.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao katika mchezo huo, uliopigwa jana Uwanja wa Uhuru ambapo timu hizo zilimaliza mchezo huo kwa kutokufungana.
Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.
Salim Kihimbwa wa Mtibwa akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Kelvin Yondani wa Yanga wakati wa mchezo huo.
Salim Kihimbwa wa Mtibwa akiendelea kuudhibiti mpira huku Kelvin Yondani wa Yanga, akijaribu kumnyang'anya mpira mchezo huo.
Obrey Chirwa wa Yanga akijaribu kuuzuiya mpira kwenye kifua huku akizongwa na Kelvin Kongwe wa Mtibwa.
Obrey Chirwa wa Yanga akimtoka na mpira Kelvin Kongwe wa Mtibwa katika mchezo huo.
Obrey Chirwa wa Yanga akipambana na Kelvin Kongwe wa Mtibwa kuwania mpira katika mchezo huo.
Issa Rashid 'Baba Ubaya' wa Mtibwa akiudhibiti mpira wa juu katika mchezo huo.
Donald Ngoma wa Yanga akiudhibiti mpira huku akizongwa na Kasian Ponera (12) wa Mtibwa.
Donald Ngoma akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumia wakati wa mcheo huo. Hadi mwisho wa mchezo huo, matokeo yalibaki kuwa 0-0.

No comments:
Post a Comment