TANGAZO


Monday, October 16, 2017

WAZIRI MKUCHIKA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTEKELEZA MAJUKUMU KWA KASI NA KUZINGATIA WELEDI

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais –Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi (wa kwanza kulia), akimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt.(Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) mapema leo kabla ya kuongea na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha ni watendaji wa Sekretarieti ya Ajira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za Sekretareti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kabla ya kuongea na watumishi na watendaji wa Sekretarieti hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu utekelezaji wa majukumu na utatuzi wa changamoto zilizopo.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais –Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) kuongea na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi (hawapo pichani).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi akifanunua hoja alizoulizwa kuhusu utendaji wa taasisi anayoiongoza mapema leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiongea na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Dkt. Henry Mambo akitoa maelezo kuhusu mafanikio na changamoto za TPSC kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb).
Watendaji wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) wakiwa katika kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akitoa ufafanuzi kuhusu kwa vyombo vya habari kuhusu umuhimu wa vikao kazi na taasisi anazoziongoza, mapema leo jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Henry Mambo (kushoto) akikabidhi ripoti ya mafanikio na changamoto kuhusu TPSC kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) leo jijini Dar es Salaam.
Mtumishi wa TPSC akiwasilisha maoni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mtumishi wa TPSC akiwasilisha maoni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.  

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amewataka Watumishi wa Umma kutekeleza majukumu yao kwa kasi; kuzingatia weledi pamoja na Sheria, Kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma nchini ili kuwa na utendaji bora wenye matokeo.

Mhe. Mkuchika (Mb) amesema hayo leo alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi anazoziongoza za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mkuchika amesema moja ya majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Umma na Utawala Bora ni pamoja na kusimamia na kuimarisha utawala bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za Uendeshaji na Usimamizi wa shughuli za utumishi wa umma. Hivyo, ni muhimu watumishi wa umma walio katika ofisi hiyo kuzingatia hayo ili kuwa mfano kwa wengine.

“Ofisi yetu ni kioo ambacho watu wote wanakitazama, hivyo watumishi wake hawana budi kuzingatia maadili katika utendaji kazi ili kuonyesha mfano kwa wengine,” Mhe. Mkuchika (Mb) amesema na kusisitiza watumishi wa umma kutenda haki, kutobagua na kuepukana na suala la
rushwa au ushawishi wanapowahudumia Watanzania.

Aidha, Mhe. Mkuchika (Mb) ameomba watumishi wa umma katika eneo lake na wengine kumpa ushirikiano wa kutosha na wa dhati katika utendaji kazi wake ili kurahisisha utendaji kazi na kuleta matokeo mazuri katika Utumishi wa Umma nchini.

“Mimi ni mgeni, nimekuja kwenu kujitambulisha na kujifunza, hivyo nitahitaji ushirikiano wa kutosha kutoka kwenu ili kurahisha utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi,” Mhe. Mkuchika amesisitiza na kuongeza mtendaji yoyote atakayeshindwa kutekeleza maelekezo yake, na kupata taarifa za huduma mbaya kutoka kwa wananchi atamfuata katika eneo lake la kazi kubaini ukweli.

Mhe. Mkuchika (Mb) ameanza ziara ya kikazi leo katika taasisi zilizo chini ya Ofisi yake kwa lengo la kujitambulisha na kuzifahamu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hizo ikiwemo kuchukua changamoto za kufanyia kazi.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA RAIS-MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA.

TAREHE 16 OKTOBA, 2017

No comments:

Post a Comment