Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea wa ujumbe wa Uongozi wa kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma ambapo amewapongeza kwa uimbaji wao na kuliombea taifa kudumisha amani.
(Picha zote na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kwaya wa Furahini Benjamini Ng’imba (wa pili kushoto) kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mlezi wa wa Kwaya wa Furahini Zakayo Munyawi (wa kwanza kushoto) kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Uongozi wa kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma ambapo amewapongeza kwa uimbaji wao na kuliombea taifa kudumisha amani.
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Mijuhu Singida, Dayosisi ya Kati kwa uimbaji wao na kuliombea taifa kudumisha amani.
Dkt. Mwakyembe amesema hayo leo mjini Dodoma alipotembelewa na Uongozi wa kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Mijuhu Singida.
“Nchi inaongozwa kwa Baraka za Mungu, nanyi kama wanakwaya mnasaidia kuongoza nchi yetu kwa kuhamasisha wananchi na jamii kuitunza na kuisimamia amani yetu” Dkt. Mwakyembe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kwaya wa Furahini Bw. Benjamini Ng’imba kwa niaba ya uongozi wa kwaya amesema kuwa wanaungana na Serikali kwa kuiombea nchi amani ili wananchi waendelee kufanya shughuli za maendeleo kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Aidha, Bw. Ng’imba ameongeza kuwa wamechukua fursa hiyo ya uimbaji kuuunga mkono juhudi za kudumisha amani na umoja miongoni mwa jamii kwa njia ya uimbaji kwa manufaa ya taifa pamoja na kizazi cha sasa na baadaye.





No comments:
Post a Comment