Wadau wa masuala ya sekta ya Ardhi
wakiwa katika picha ya pamoja.
Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA
kutoka Wizara ya Ardhi akitoa ufanunuzi juu ya ujenzi wa Mfumo unganishi wa
taarifa za sekta ya Ardhi (ILMIS).
Wadau wa Sekta ya Ardhi
wakisiliza taarifa kuhusu mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya Ardhi nchini
kutoka kwa mtaalamu (hayuko pichani).
|
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi imeendesha warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa masuala ya sekta ya ardhi
nchini kuhusu mifumo mbalilmbali inavyotumika katika kutoa huduma kwa wananchi.
Akifungua warsha hiyo Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Ardhi Dkt. Moses Kusiluka alisema, hadi sasa wizara inatumia mfumo
zaidi ya mmoja kutoa huduma za kila siku kwa mwananchi. Uwepo wa mifumo hiyo katika utoaji huduma za
sekta ya ardhi ni muhimu kwa ajili ya kurahisisha huduma. Ili kufikia malengo,
ni lazima kuwepo na mfumo mmoja utakaounganisha mifumo yote hiyo kwa lengo la
kuongeza ufanishi na kuboresha huduma.
Uundaji wa mfumo unganishi wa taarifa za
sekta ya ardhi (Intergrated Land Management Information System, ILMIS) unatekelezwa
na Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishiriana na wataalamu
kutoka kampuni ya IGN FI kwa udhamini wa Benki ya Dunia. Uundaji huu ulishaanza na kwa sasa mfumo uko
katika hatua ya majaribio.
Dhumuni kuu la uundaji mfumo unganishi wa
taarifa za sekta ya ardhi ni kuimarisha usalama katika umiliki wa ardhi kwa
kuboresha usahihi katika taarifa za ununuzi ardhi, usajili, upimaji na pia
katika kusimamia ardhi kwa ujumla wake.
Utekelezaji wa Mfumo unganishi wa taarifa
za sekta ya ardhi (ILMIS), utahusisha mambo mbalimbali kama vile njia rahisi na
rafiki ya kusimamia uundaji na uendelezaji wa mfumo wenyewe, majaribio ya mfumo katika utekelezaji,
ubadilishaji wa taarifa za ardhi zilizopo mfano taarifa za upimaji na ramani, hatimilki
na kuziweka katika mfumo.
Naye Msajili Msaidizi wa Hati, Appolo
Laizer alisisitizia umuhimu wa utumiaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya
ardhi (ILMIS) kwa wadau wa sekta ya ardhi alipokuwa akielezea jinsi hatimilki
zitakavyotolewa na mfumo huo.
Alisema, utoaji wa hati kupitia mfumo
utaongeza usalama katika nyaraka za umiliki, huduma sahihi, salama na kwa
unafuu zaidi. Mfumo utapunguza muda wa kuhakiki taarifa katika uhamisho wa
milki kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kuongeza ulinzi kwenye maeneo
yaliyotengwa kama hifadhi ya barabara, misitu au maeneo ya wazi.
Utoaji wa hatimilki kwa kutumia mfumo
utasaidia sana kupunguza kama sio kumaliza kabisa migogoro ya ardhi kwa kulinda
umiliki wa mwananchi. Pia mfumo utaondoa migogoro ya umilikishaji wa hati kwa
mtu zaidi ya mmoja pamoja na kuongeza ulinzi wa hatimilki katika taasisi za
kifedha.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA
YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

No comments:
Post a Comment