Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo cha
Ushirika Moshi, Dkt. Lucas Mataba (kushoto), akitoa salam kwa Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba, Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (katikati), katika maadhimisho ya makazi duniani yaliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo wa kwanza kushoto
ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala.(Picha zote na Paschal dotto- Maelezo)
Mkurugenzi wa Mipangomiji Profesa John Lupala (kulia), akitoa maelezo kwa wadau wa nyumba na makazi katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula na kushoto ni Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi, Dkt.Lucas Mataba.
Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akihutubia katika hafla ya maadhimisho ya 32 ya makazi duniani, yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Urasimishaji Makazi, Bi. Beritha Mlonda akiwasilisha makala ya urasimishaji makazi katika maeneo yaliyoko kwenye mkakati wa mpango wa makazi bora kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam hivi leo.
Wadau wa nyumba na makazi wakifuatilia mkutano wa maadhimisho ya 32 ya makazi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “sera za nyumba ,nyumba za gharama nafuu”.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (katikati) kulia ni Mkurugenzi wa Mipangomiji, Profesa John Lupala na kushoto ni Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi Dkt.Lucas Mataba wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa nyumba na makazi wa bodi ya mwenge Jijini Dar es Salaam katika madhimisho ya 32 ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo.




No comments:
Post a Comment