Bayern Munich itatoa tangazo kuhusu hatma ya kocha Carlo Ancelotti baadaye siku ya Alhamisi.
Bodi ya timu hiyo ilikutana baada ya kichapo cha 3-0 dhidi ya PSG siku ya Jumatano.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 alichukua mahala pake Pep Guardiola mwanzo wa msimu wa 2016-17.
Ancelotti aliisaidia Bayern kushinda kombe la Bundesliga , lakini klabu hiyo ikaweza kufika katika awamu ya makundi ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Walishindwa kufika katika fainali ya DFB baada ya kushindwa 3-2 na Borussia Dortmund.
Ancelotti ameshinda kombe la vilabu bingwa mara tatu mbali na mataji ya ligi nchini Itali, Uhispania, Uingereza na Ujerumani.


No comments:
Post a Comment