Mashabiki wa Yanga wakifuatilia matukio wakati wa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya timu hiyo na Simba, uliochezwa juzi Agost 23 jijini Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya kumaliza dakika 90 za kawaida bila kufungana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mashabiki wa Simba wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya timu hiyo dhidi ya Yanga, juzi Agost 23 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Simba wakiingia uwanjani tayari kwa mchezo huo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, juzi Agost 23, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo, juzi Agost 23, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Simba wakipiga picha ya pamoja ya kumbukumbu kabla ya mpambano huo, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Yanga wakipiga picha ya pamoja ya kumbukumbu kabla ya mpambano huo, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Haruna Niyonzima wa Simba (kulia), akimfuta Andrew Vicent wa Yanga wakati wa mchezo huo.
Ally Shomari wa Simba akijaribu kumpiga chenga Gadiel Michael wa Yanga wakati wa mchezo huo.
Gadiel Michael wa Yanga,akijaribu kuutoa mpira miguuni mwa Ally Shomari wa Simba.
Shiza Kichuya wa Simba akiudhibiti mpira huku Donald Ngoma wa Yanga akiwa amedondoka chini.
Emmanuel Okwi (kushoto) wa Simba akiwania mpira na Kelvin Yondani wa Yanga.
Emmanuel Okwi (kushoto) wa Simba akiupiga mpira huku akifuatwa na Gadiel Michael wa Yanga.
Laudit Mavugo wa Simba akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Gadiel Michael wa Yanga.
Emmanuel Okwi wa Simba akimtoka Kelvin Yondani wa Yanga, katika mchezo huo.
Kelvin Yondani akiaribu kumdhibiti Emmanuel Okwi wa Simba.
Hadi dakika ya 38 timu hizo zilikuwa hazijafungana.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo.
Haruna Niyonzima wa Simba akiwatoka wachezaji wa Yanga, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo. Hadi zilipotimia dakika 90 za mchezo huo, timu hizo hazikuweza kufungana na ndipo uamuzi wa kupiga penalti 5, 5 ukaanza.
Hapa golkipa wa Yanga, Youthi Rostand akishindwa kudaka moja ya penalti alizopigiwa kwenye lango lake katika mchezo huo. Baadaye aliokoa penalti ya tano ya Simba iliyopigwa na Mohammed Hussein.
Golkipa Aishi Manula wa Simba naye akishindwa kudaka moja ya penalti alizopigiwa kwenye lango lake katika mchezo huo, huku akiwa ameokoa penalti iliyopigwa na Kelvin Yondani wa Yanga.
Mohammed Hussein wa Simba akienda kupiga penalti ya tano ya Simba ambayo ilidakwa na golkipa Youthi Rostand wa Yanga.
Hapa golkipa Youthi Rostand wa Yanga, akidaka penalti iliyopigwa na Mohammed Hussein. Kisha Juma Mahadhi wa timu hiyo, akipoteza penalti yake ya sita na kutoa nafasi kwa Simba kuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.
Mchezaji Mohammed Ibrahim wa Simba akiweka mpira kupiga penalti ya sita kwa timu hiyo, ambayo alifunga kistadi na hivyo Simba kushinda mchezo huo kwa mikwaju 5 kwa 4 na kunyakuwa Ngao ya jamii.
Simba wakishangilia ushindi huo
Ubao wa matokeo ukionesha Simba imeshinda penalti 5 na Yanga kupata 4.
Wachezaji wa Simba wakishangilia na kupongezana baada ya kupata ushindi huo.
Simba wakivalishwa medali za dhahabu, huku wenzao, Yanga wakiambulia za shaba.
Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (kulia), akimkabidhi Nahodha wa Simba, Method Mwanjale Ngao ya Jamii.

No comments:
Post a Comment