TANGAZO


Thursday, August 10, 2017

Korea Kaskazini: Tuna mpango wa kushambulia kisiwa cha Marekani cha Guam siku chache zinazokuja

South Korean soldier walks past TV showing a graphic of the distance between North Korea and Guam at a railway station in Seoul on 9 August 2017

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKorea Kaskazini inasema mpango wake ya kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam
Korea Kaskazini inasema mpango wake ya kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, utakuwa tayari hivi karibuni huku majibizano ya kivita kati yake na Marekani yakiendelea.
Vyombo vya habari vilisema kuwa makombora ya Hwasong-12 yatapita anga ya Japan na kuanguka baharini karibu kilomita 30 kutoka kisiwa cha Guam ikiwa mpango huo utaidhinishwa na Kim Jong-un.
Korea ilipuuzia onyo la Donald Trump kuwa itashambuliwa vikali.
Marekani imeionya Korea Kaskazini ikisema kuwa vitendo vyake vinamaanisha kuwa huo utakuwa mwisho wa utawala wa nchi hiyo.
Map showing Guam
Image captionKisiwa hicho kilicho bahari ya Pacific cha Guam ndiko ziliko kambi za jeshi za Marekani na watu 163,000
Waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis alisema kuwa Korea Kaskazini itashindwa vibaya ikiwa itaingia vitani na Marekani na washirika wake.
Korea Kaskazini ilitangaza siku ya Jumatano kuwa inachora mipango ya kufanya mashambulizi ya makombora katika kisiwa kilicho bahari ya Pacific cha Guam kilicho na kambi za jeshi la Marekani na watu 163,000
Taarifa iliyotolewa baadaye ilisema kuwa jeshi litakamisha mpango huo ifikapo kati kati mwa mwezi Agosti na kupeleka kwa kiongozi wao Kim Jong-un kuidhinishwa.

No comments:

Post a Comment