Meneja ujenzi wa
kampuni ya BAM International, Bw. Rey Blumrick akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wa hatua iliyofikiwa
kwenye ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa jengo hilo leo mchana.
Meneja ujenzi wa kampuni ya BAM International, Bw. Rey Blumrick akifafanua Jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akiwa katika
pichaa ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), na watendaji mbalimbali mara baaada ya kukagua ujenzi wa Jengo la 3 la
Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo mchana.
Muonekano wa sehemu ya Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kukamilika kwake kutawezesha jengo hilo kuhudumia abiria wapatao milioni 8 na nusu kwa mwaka.
WAZIRI wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua ujenzi wa jengo la
Tatu la Abiria la uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na kuelezea
kuridhishwa kwake kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
Akizungumza mara baada
ya kukagua ujenzi huo Waziri Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi BAM
International anayejenga jengo hilo kuwa Serikali italipa madai yake kwa wakati
kwa kadri atakavyoyawasilisha.
“Nia yetu ujenzi huu
ukamilike ifikapo Septemba mwakani, hivyo tunamtaka mkandarasi kuongeza kasi ya
ujenzi na wasimamizi kumsimamia kikamilifu ili vifaa vinavyofungwa katika jengo
hilo viwe na ubora uliokusudiwa na vidumu kwa muda mrefu”, amesisitiza Profesa
Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema
kukamilika kwa jengo la tatu la abiria la uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kutawezesha
uwanja huo kuweza kuhudumia abiria wapatao milioni 8 na nusu kwa mwaka na hivyo kukuza uchumi wa nchi
kwa kuwezesha watalii na wageni wengi zaidi kufika nchini.
Naye Mwenyekiti wa Bodi
ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Profesa Ninatubu
Lema amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi huo unasimamiwa kikamilifu
na utamalizika kwa wakati.
“Kama wasimamizi
tumejipanga kuhakikisha zoezi la ufungaji vifaa katika jengo hili, linakamilika
kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa,” amesisitiza Prof. Lema.
Naye Meneja ujenzi wa
BAM International, Bw. Rey Blumrick amesema kazi iko katika hatua nzuri na
itakamilika kwa wakati.
Mradi wa ujenzi wa
jengo la tatu la abiria ni sehemu ya uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere lengo likiwa ni kuwezesha ndege na abiria wengi kutumia
uwanja huu na kuhuisha sekta ya usafiri wa anga hapa nchini.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:
Post a Comment