Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu kuwataka wananchi kujitokeza kuchangia damu. Waziri Mwalimu alitoa ombi hilo, wakati alipotembelea katika tukio la uchangiaji damu lililofanyika Makao Makuu ya benki ya KCB jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu kuwataka wananchi kujitokeza kuchangia damu.
Na Mwandishi wetu
WATANZANIA
waaswa kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara ili kuondokana na tatizo
la vifo vinavyotokana na upungufu wa damu hasa kwa kina mama wajawazito nchini
wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea katika tukio
la uchangiaji damu lililofanyika Makao makuu ya benki ya KCB jijini Dar es Salaam.
“Marufuku kwa mtoa huduma yeyote wa afya kuuza
damu mgonjwa kwani wananchi wanachangia
damu bure kwa manufaa yao ya baadae aidha kwa wao wenyewe au ndugu zao” alisema
Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amewaagiza Waganga Wafawidhi wa
mikoa kuhakikisha wanaweka mabango yanayoonyesha kuwa damu ni bure kwa wagonjwa
wote wanaohitaji huduma hiyo bila ya kubagua mwananchi yeyote.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa mwananchi
yeyote mwenye umri wa miaka 18, mwanamke asiye mjamzito wala kunyonyesha na asiyekua mgonjwa kama vile
kisukari,saratani na mgonjwa wa moyo
anaweza kuchangia damu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya
KCB nchini Bw. Cosmas Kimario amesema kuwa wameamua kuaandaa uchangiaji wa damu
ili kuisadia Serikali katika sekta ya Afya hususani katika kupunguza vifo vinavyotokana
na upungufu wa damu.

No comments:
Post a Comment