TANGAZO


Wednesday, May 24, 2017

RAIS MAGUFULI AKABIDHIWA RIPOTI YA KWANZA KUHUSU UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI (MAKINIKIA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya kupokea ripoti ya kamati ya kwanza ya iliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha madini kilichopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) uliokamatwa katika bandari ya Dar es Salaam ukiwa katika makontena 277 tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia), Profesa Abdulkarim Hamis Mruma akiwasilisha ripoti yao mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) wakati hafla ya kuwasilisha ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo ya watu wanane iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ripoti kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia), Profesa Abdulmalik Mruma katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipitia ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa AbdulKarim Hamis Mruma (kushoto) katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Wazri Mkuu Kassim Majaliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (watatu kutoka kulia).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata ufafanuzi  kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia), Profesa Abdulkarim Hamis Mruma kuhusu baadhi ya takwimu zilizopo katika ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kululia ni Wazri Mkuu Kassim Majaliwa.  
Wajumbe wa Kamati ya Kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) wakiwa tayari kwa kuwasilisha ripoti yao katika hafla iliyofanyika Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Wajumbe wa Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Profesa Abdulkarim Hamis Mruma, wengine ni Profesa Justianian Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dk Yusuf Ngenya, Dk Joseph Yoweza Philip, Dk Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akisalimiana na Viongozi wa Vyama vya Siasa alipokutana nao katika hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo.
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania – JWTZ, (CDF) Venance Mabeyo akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji George Masaju alipokutana nao katika hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.  
PIX5: Wasanii wa Kundi la Tanzania All Stars wakitumbuiza wimbo wa kuhamasisha uzalendo wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.(Picha zote na Frank Shija - Maelezo)

No comments:

Post a Comment