Mkuu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Kamishna Jenerali Thobias Andengenye akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa wananchi kutoa taarifa za matukio ya moto na ajali kwa wakati ili hatua za uokoaji ziweze kuchukuliwa kwa wakati muafaka, Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Bw.Casmir Ndambalilo na kulia ni Msemaji wa Jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano
Mkuu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Kamishna Jenerali Thobias Andengenye Leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mikakati ya
Jeshi hilo kuboresha huduma wanazotoa
kwa kushirikisha wadau wa Maendeleo.
Na Nuru Juma, Maelezo
JESHI la Zimamoto
nchini limedhamiria kuimarisha huduma zake na limefanikiwa kutoa elimu kwa wananchi
zaidi ya laki tisa juu ya namna ya kuzuia majanga ya moto na maafa.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Jeshi la Zima Moto na
Uokoaji nchini Kamishna Jenerali Thobias Andengenye alitoa wito kwa wananchi
kuwasiliana na jeshi hilo mara tu panapotokea ajali au majanga ili kuharakisha
uokoaji.
Kamishna Jenerali
Andengenye alisema Jeshi hilo limeweza kutoa elimu kwa wananchi kupitia njia
mbalimbali zikiwemo vituo vya redio, televisheni na magazeti ili kuwaelimisha
zaidi kuhusu hatua za kuchukua mara yanapotokea majanga.
“tunaendelea kutoa elimu kwa watanzania na
toka Januari mwaka jana tumeweza kufikia takribani watu laki tisa na
tunaendelea kuweka programu ya kuzifikia taasisi za elimu kama vile shule za
msingi na sekondari.” alisema Andengenye.
Aliongeza kuwa Jeshi
hilo limekuwa likifanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo mbali mbali
hususan majengo kuhakikisha kuwa hatua zote za tahadhari zinachukuliwa kuepusha
na kukabiliana na ajali na majanga yanayoweza kutokea.
Kamishna Jenerali
huyo alibainisha kuwa kwa sasa Jeshi lake limefanikiwa kuwa na vituo katika
viwanja vyote vya ndege nchini na jitihada zaidi zinafanyika ili kuhakikisha Jeshi
hilo linakuwa na ofisi zake katika maeneo yote nchini.
Alieleza pia kuwa katika
kuongeza ufanisi, Jeshi hilo linatarajia kuajiri watumishi zaidi kulingana na
mahitaji ya jeshi hilo hasa kwa kuzingatia vituo vipya ambavyo jeshi hilo
inatarajia kuvifungua.

No comments:
Post a Comment