TANGAZO


Tuesday, February 7, 2017

Kiranja wa upinzani bungeni Tanzania akamatwa

Mbunge wa Singida mashariki nchini Tanzania Tundu LissuHaki miliki ya pichaBUNGE
Image captionMbunge wa Singida mashariki nchini Tanzania Tundu Lissu
Kiranja wa bunge upande wa upinzani na mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu alikamatwa siku ya Jumatatu nje ya bunge na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kujibu madai yasiojulikana
Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen nchini humo, kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe {Hai Chadema} aliwaambia waandishi kwamba bado hawajajua sababu za kukamatwa kwake.
''Ni kweli alikamatwa na amesafirishwa hadi Dar Es Salaam.Tayari tumewasiliana na wakili wetu na analifuatilia swala hilo''.
Kulingana na Gazeti hilo kamanda wa polisi mjini Dodoma Lazaro Mambosasa alithibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo na kusema kuwa wamepokea agizo kutoka Dar es Salaam, ''tumemkamata kwa uhalifu aliotekeleza na maandalizi ya kumsafirisha yanaendelea'', alisema katika simu.
Aidha gazeti hilo limemnukuu dereva wa Bw Lissu, Simon Makira akisema mwajiri wake alikamatwa mwendo wa saa kumi na moja jioni alipokuwa akitoka katika eneo la bunge ,''alipokuwa akitoka bungeni alifuatwa na maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia nguo za kawaida waliosema wamekuja kumkamata''.
''Aliwauliza kwa nini walitaka kumkamata na iwapo walikuwa na kibali. Hakuonyesha chochote isipokuwa vitambulisho vyao na wakamwambia anatakiwa kuwasilishwa mahakamani siku ya Jumanne''.
''Baadaye alipelekwa hadi ndani ya gari'' na kuondoka.

No comments:

Post a Comment