Mshauri wa
Sheria wa Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) Bw. Ikunda Mkenda akiwaeleza
waandishi wa habari (hawapo pichani)Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya
Baraza hilo katika kushughulikia rufani za mashauri yanayowasilishwa kutokana na
maamuzi ya Tume ya Ushindani(FCC) pamoja na Mamalaka za udhibiti kama
EWURA,TCAA,SUMATRA na TCRA. kulia ni Mchumi Mwandamizi wa Baraza hilo Bw. Nonge
Ally.(Picha zotr na Frank Mvungi-Maelezo)
Mchumi Mwandamizi wa Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) Bw. Nonge Ally akifafanua kwa waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu huduma zinazotolewa na Baraza hilo katika kuhakikisha kuwa kuna ushindani wenye tija katika soko. Mshauri wa Sheria wa Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) Bw. Ikunda Mkenda.
Mshauri wa Sheria wa Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) Bw. Ikunda Mkenda akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Baraza la Ushindani Tanzania (FCT)
leo Jijini Dar es Salaam.
Frank Mvungi-Maelezo
BARAZA la ushindani
Tanzania (FCT) lapokea na kushughulikia mashauri 139 kati 164 yaliyowasilishwa
kutokana na maamuzi ya Tume ya Ushindani pamoja na Mamlaka za Udhibiti ili
kuweka mazingira ya usawa katika soko nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mshauri wa Sheria wa Baraza hilo Bw. Kunda
Mkenda wakati wa mkutano na waandishi habari Leo Jijini Dar es Salaam.
Akifafanua suala hilo
Mkenda amesema kuwa dhamira ya Baraza hilo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na
ushindani wenye tija kwenye soko.
Akizungumzia majukumu
ya Baraza hilo Mkenda alisema kuwa Baraza hilo linaweza kubadilisha uamuzi wa
Tume ya ushindani au Mamlaka ya udhibiti ili kuweka mazingira ya usawa katika utoaji wa
huduma katika soko.
“Jukumu kubwa ni
kukuza na kulinda ushindani wa haki na kumlinda mlaji dhidi ya matokeo ya
ukiritimba na tabia potofu katika soko ili kuepusha athari katika uchumi” Alisisitiza Mkenda.
Pia, aliongoza kuwa
Baraza hilo linaweza kutoa adhabu, faini, amri, tamko au kuamuru kulipwa fidia
kutokana na hasara anayokuwa amepata mlalamikaji au muwasilisihaji wa rufani
katika Baraza.
Aidha, Mchumi
Mwandamizi wa Baraza hilo Bw. Nonge Aly liongeza kuwa wananchi wanalo jukumu
kubwa la kutumia huduma zinazotolewa na
Baraza hilo.
Baraza la Ushindani
ni Chombo kilichoanzishwa na serikali chini ya kifungu cha 83 (1) cha Sheria ya
ushindani namba 8 ya mwaka 2003.

No comments:
Post a Comment