Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Iddi wakati alipowasili Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar jana, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipamgo wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed. (Picha zote na Ikulu- 06/01/2017, kwa hisani ya Zanzinews)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Bara Dkt. Ashatu Kijaji, mara alipowasili Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar jana, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipamgo Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bi. Elizabe Ann Talbert (kulia) wakifungua pazia kuashiria Uwekaji wa jiwe la Msingi jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar huko Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi jana ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar, uliowekwa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein huko Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mkandarasi wa Ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar Ndg. Edwin Shitindi kutoka alipokuwa akitoa maelezo ya Kitaalam kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupi pichani) baada ya kuliweka jiwe la msingi jengo hilo jana, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake baada ya kuliweka jiwe la msingi jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar jana, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipamgo Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed.







No comments:
Post a Comment