TANGAZO


Saturday, December 24, 2016

WIZARA YA HABARI YATOA TAARIFA ZA VIFO

 Modest Mfutakamba Mfilinge

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, wapiga picha pamoja na Wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha mwanahabari na mpiga picha Mpoki Bukuku kilichotokea jana tarehe 23 Desemba, 2016 katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Nape Nnauye pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanahabari huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini.

Mhe. Waziri Nape amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari huyo na ameeleza kuwa, kifo chake ni pigo katika tasnia ya habari hususani katika picha kwasababu Marehemu wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya Majira, Business Times, The Guardian, Nipashe na Mwananchi na The Citizen.

Wakati huo huo Mhe. Waziri ametuma salamu za rambirambi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na familia kufuatia kifo cha mtumishi wake Bw. Modest Mfutakamba Mfilinge kilichotokea usiku wa kuamkia leo 24 Desemba, 2016.

Mungu azilaze roho za Marehemu mahali pema peponi. Amina.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Dar es Salaam.

24 Desemba, 2016.

No comments:

Post a Comment