TANGAZO


Sunday, December 4, 2016

Trump: Alec Baldwin ananiigiza vibaya

Rais mteule wa Marekani Donald Trump na mtu anayemwigiza Alec Baldwin
Image captionRais mteule wa Marekani Donald Trump na mtu anayemwigiza Alec Baldwin
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amelalamika juu ya kipindi che televisheni cha vichekesho kwa jina Saturday Night Live.
Amesema anaigizwa vibaya sana na mchezaji Alec Baldwin.
Bw Trump kaandika kwenye twitter, kwamba kipindi hicho, hakitazamiki, na kinalemea upande mmoja kabisa.
Katika kichekesho, Bw Trump anaoneshwa kashughulika sana na Twitter, hata hawezi kuzingatia sera za mashauri ya nchi za nje.
Donald Trump na mtu anayemuigiza Alec Baldwin kuliaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionDonald Trump na mtu anayemuigiza Alec Baldwin kulia
Na katika kichekesho, mmoja anasema rais mteule anaandika sana kwenye Twitter ili kusahaulisha vyombo vya habari, visitazame mawaziri alioteuwa karibu na masilahi yake ya kibiashara.

No comments:

Post a Comment