TANGAZO


Wednesday, December 7, 2016

Trump akataa ndege mpya za Air Force One

Donald TrumpImage copyrightREUTERS
Image captionBw Trump amesema gharama ya ndege hizo ni ya juu mno
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amesema anataka kufuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force One ambazo hutumiwa na marais wa Marekani.
Wiki sita kabla yake kuingia madarakani, aliandika kwenye Twitter: "Boeing wanaunda ndege mpya aina ya 747 Air Force One za kutumiwa na marais siku zijazo, lakini gharama yake imezidi, zaidi ya $4 bilioni. Futa oda hiyo!"
Serikali ya Marekani iliingia kwenye mkataba na kampuni ya Boeing wa kuundwa kwa ndege mbili au zaidi za kuwabeba marais.
Ndege hizo zilitarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka 2024.
Hisa za kampuni hiyo ya ndege ya Boeing zilishuka kwa zaidi ya 1% baada ya ujumbe huo wa Trump kwenye Twitter, ingawa zilijikwamua baadaye alasiri.
Bw Trump hatarajiwi kutumia ndege hizo mpya, iwapo hatashinda uchaguzi wa muhula wa pili mwaka 2020.
Rais huyo mteule pia alitangaza Jumanne kwamba benki ya SoftBank ya Japan imekubali kuwekeza $50bn (£39.4bn) nchini Marekani, hatua inayotarajiwa kuunda nafasi 50,000 mpya za ajira.
Bw Trump alifichua mpango huo baada ya kukutana na afisa mkuu mtendaji wa SoftBank Masayoshi Son katika afisi yake jumba la Trump Tower.
Ndege ya kibinafsi ya Bw Trump ni aina ya Boeing 757Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionNdege ya kibinafsi ya Bw Trump ni aina ya Boeing 757
"Masa alisema hawangefanya hivi iwapo sisi (Trump) hatungeshinda uchaguzi!" Bw Trump aliandika kwenye Twitter.
Bw Trump kwa sasa anatumia ndege yake binafsi, lakini atakapokuwa rais atahitajika kutumia ndege za Air Force One, ambazo zimeimarishwa mifumo ya usalama, ulinzi na mawasiliano.
Huwa anajivunia sana ndege yake aina ya Boeing 757 iliyoandikwa jina Trump na alijiringa akihojiwa na Rolling Stone mwaka jana kwamba ndege yake ni "kubwa kuliko Air Force One, ambayo imo hatua moja chini kwa kila namna".
Kwingineko:
  • Katika hotuba yake ya mwisho kuhusu usalama wa kitafa, rais Obama amewaomba raia Marekani kutopoteza muelekeo wa maadili yalioiunda nchi hiyo. Amesisitiza msimamo wake kupinga mateso ikiwemo mfumo wa kuwafunika watuhumiwa kitambara usoni huku wakimwagia maji na kukatizwa pumzi - mbinu ambayo mrithi wake Donald Trump ameitetea katika siku za nyuma.
  • Bw Trump aliuza hisa zake zote mwezi Juni, msemaji wake alisema, katika hatua ambayo huenda ikapunguza shutuma kuhusu mwingiliano wa maslahi
  • Wabunge wa Republican katika Bunge la Congress walisema watapinga mpango wa Trump wa kuweka mfumo mkali wa ushuru kwa kampuni za Marekani zinazohamia ng'ambo
  • Mjumbe wa Republican atakayewakilisha jimbo la Texas katika Kura za Wajumbe ameapa kuondoa uungaji mkono wake kwa Bw Trump wajumbe watakapokutana kupiga kura za urais wiki ijayo
  • Makamu wa Rais Joe Biden, 74, alidokeza kwamba huenda akawania urais kwa mara ya tatu, mwaka 2020.

Gharama

Mwandishi wa BBC aliyepo new York Zoe Thomas, anasema kama rais na amiri jeshi mkuu, Donald Trump, atakuwa na mamlaka ya kufuta mkataba wa Marekani na Boeing wa ununuzi wa ndege mpya.
Lakini akifanya hivyo, hilo huenda likagharimu mlipa kodi wa Marekani pesa zaidi katika kipindi ambacho rais huyo anatarajiwa kuwa akifanya juhudi kubana matumizi.
Marekani tarayi imetia saini mkataba wa ununuzi wa ndege hizo na Boeing ambao ni wa $170m (£134m; €158m).
Pesa zaidi zinatarajiwa kutolewa kulipia ndege hizo mbili.
Inakadiriwa kwamba gharama kamili itakuwa $3.2bn.
Iwapo Bw Trump atafuta mkataba huo, basi Marekani huenda ikapoteza pesa ambazo tayari imetia saini mkataba kwamba italipa.
Rais Obama akiwa katika Air Force OneImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionRais Obama akiwa katika Air Force One

Air Force One ikiwa Maryland 6 Desemba 2016Image copyrightREUTERS

Afisi inayopaa

  • Kimsingi, "Air Force One" ni jina ambalo hutumiwa kurejelea ndege zinazombeba rais wa Marekani. Sasa, hutumiwa kwa ndege mbili aina ya Boeing 747-200B
  • Ndege hizo zinaweza kuongeza mafuta zikiwa bado zinaendelea na safari na zina mitambo ya kisasa na salama zaidi ya mawasiliano. Mara nyingi huelezwa kama Afisi ya rais inayopaa
  • Ndani yake, rais na wanaosafiri naye huwa na nafasi ya futi mraba 4,000 (400 mita mraba) ya sakafu katika ghorofa tatu
  • Ina chumba kamili cha rais pamoja na vyumba vya washauri wake, maafisa wa usalama wa Secret Service na wanahabari wanaosafiri na rais
  • Kuna chumba cha matibabu pia ambacho kinaweza kutumiwa kwa upasuaji, na huwa hapakosi daktari
  • Ina jikoni mbili ambazo zinaweza kuhudumia watu wawili kwa wakati mmoja

No comments:

Post a Comment