Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Dkt. Ayoub Rioba (kulia), akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma baada kuwa mshindi wa pili kutoka kwa kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw .Shogolo Msangi kushoto wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Mapato kutoka kampuni ya kutengeneza sementi (Tanga Cement Plc) Bw. Pieter De Jager wa pili kulia akiwa ameshika tuzo ya washindi wa jumla kwenye masindano ya wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Shogolo
Msangi (katikati waliokaa), akiwa katika
picha ya pamoja na washindi wa uwasilishaji bora wa mapato wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa
mwaka 2015 iliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Na
Ally Daud-MAELEZO
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzo ya
utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma
zilizoandaliwa na Bodi ya
Ukaguzi na Wahasibu (NBAA) kwa mwaka 2015.
Akipokea tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa Idara ya
Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme amesema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha
yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na
Wahasibu (NBAA).
“Tumefanya vizuri na tumepata tuzo kwa kushika
nafasi ya kwanza kutokana na kuwasilisha
vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya
uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi
ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA)” alisema Bi. Mndeme.
Aidha Bi. Mndeme amesema kuwa tuzo hiyo ni chachu
kwa TRA itayofanya waendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa
mapato ili kusaidia nchi kupata huduma bora za jamii kwa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipakodi TRA Bw. Richard Kayombo amesema kuwa huo ni uthibitisho kwamba TRA
inafanya kazi kwa ueledi na uwazi kupelekea
kupata tuzo ya heshima.
Katika mashindano hayo Shirika la Utangazaji la
Taifa (TBC) wameibuka washindi wa pili huku kampuni inayotengeneza Sementi (Tanga Cement Plc) wakiibuka kuwa washindi wa
jumla kwenye tuzo hizo.

No comments:
Post a Comment