Mashabiki wa timu ya Simba, wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya JKT Ruvu, ulikuwa ukichezwa Uwannja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam jana. Katika mchezo huo, Simba ilishinda bao 1-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Pastory Athanas wa Simba akitafuta mbinu ya kumtoka Frank Nchimbi wa JKT Ruvu wakati wa mchezo huo.
Pastory Athanas wa Simba akipiga mpira mbele ya Kassim Kisengo wa JKT Ruvu.
Frank Nchimbi wa JKT Ruvu akiwania mpira na Pastory Athanas wa Simba wakati wa mchezo huo.
Frank Nchimbi wa JKT Ruvu akikimbia na mpira huku akifuatwa na Pastory Athanas wa Simba.
Golikipa wa JKT Ruvu, Hamis Seif akiruka juu kuupiga pira ngumi karibu na nje ya eneo la 18, hatua iliyomfanya kushindwa kurudi langoni kwake na kusababisha timu ya Simba kujipatia bao la pekee na la ushindi katika mchezo huo, uliokuwa wa vuta nikuvute.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la ushindi lililofungwa na Mzamiru Yassin baada ya golikipa wa JKT Ruvu kutoka langoni kwake na kwenda kuupiga mpira ngumi karibu na nje ya eneo la 18 la lango lake.
Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kufanikiwa kufunga bao hilo pekee katika mchezo huo.
Ubao wa matangazo ukionesha Simba bao 1 na JKT Ruvu 0.
Mashabiki wa Simba wakishangilia bao hilo.
Makocha wa Simba wakiwa kwenye bechi lao, wakifuatilia mchezo huo.
Mohamed Ibrahim wa Simba akiwa karibu na golikipa wa JKT Ruvu, Hamis Seif aliyelala na mpira.
Shiza Kichuya wa Simba akiwatoka wachezaji wa JKT Ruvu.
Frank Nchimbi wa JKT Ruvu na Pastory Athanas wa Simba, wakiwania mpira.
Said Ndemla (13) wa Simba na Yussuf Chuma wa JKT Ruvu wakiwania mpira wa juu.
Said Ndemla (katikati) wa Simba akiudhibiti mpira huku akizongwa na Yussuf Chuma (4) na Frank Nchimbi wa JKT Ruvu.
Mashabiki wa Simba wakitoka nje ya Uwanja wa Uhuru kwa furaha baada ya timu yao kushinda bao 1 kwa 0 dhidi ya JKT Ruvu.
Mashabiki wa Simba wakitoka nje ya Uwanja wa Uhuru kwa furaha baada ya timu yao kushinda bao 1 kwa 0 dhidi ya JKT Ruvu.

No comments:
Post a Comment