Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi Beatrice Fungamo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto akikabidhi kwa niaba ya Rais zawadi ya Sikukuu kwa Msimamizi wa Kituo cha watoto Msimbazi arc diocese cha Dar es Salaam leo jijini Dare es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi Beatrice Fungamo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto akikabidhi kwa niaba ya Rais zawadi ya Sikukuu kwa Msimamizi wa Kituo cha Watoto cha Dar Al Arqum International Islamic Relief Organisation leo jijini Dare es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi Beatrice Fungamo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto akikabidhi kwa niaba ya Rais zawadi ya Sikukuu kwa Msimamizi wa Kituo cha Watoto Mburahati leo jijini Dare es Salaam.
Na
Anthony Ishengoma
RAIS John Magufuli ametoa zawadi yenye thamani ya
shilingi 8,475,00 kwa watu walio katika
makundi maalum wakiwemo watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee
wanaohudumiwa katika makazi ili waweze kusherehekea sikuu ya krismass ya mwaka
2016 na mwaka mpya 2017.
Akikadidhi zawadi hizi kwa
niaba yake Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi Beatrice
Fungamo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto
amesema ni utaratibu wa kawaida kwa viongozi Wakuu
wa Nchi yetu kuwapatia makundi haya maalum zawadi ya Siku Kuu Krismass ya mwaka
huu na mwaka mpya.
Zawadi zilizotolewa kwa thamani hiyo ya fedha ni vyakula
kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha kufurahi na
kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.
Zawadi
hizi zimetolewa kwa vituo 7 katika Mkoa wa Dar es Salaam, vituo viwili kutoka Zanzibar
na Makazi ya Wazee katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Tanga,
Ruvuma, Shinyanga, Singida, Mwanza, Lindi, Mtwara, Kagera, Mara na
Morogoro.
Bi.
Beatrice Fungamo amevitaja vituo hivyo kutoka mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni Makao
ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto Msimbazi, Kituo
cha Watoto Dar Al Arqum, Makao ya Watoto Mburahati, Makao ya Watoto Kijiji cha
Furaha, Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Upanga na Makazi ya Wazee Wasiojiweza
na wenye Ulemavu Nunge, Kigamboni.
Aidha
kutoka Zanzibar ni Kituo cha Watoto
Mabaoni - Chakechake, Pemba na Makazi
ya wazee wasiojiweza Sebleni – Unguja ikiwemo makambi ya wazee kutoka mikoa
yote ya Tanzania Bara yenye makambi ya Wazee.

No comments:
Post a Comment