TANGAZO


Thursday, December 22, 2016

Mourinho aomba kuifunza Man United kwa muda mrefu

Mourinho ataka kuifunza Man United kwa muda mrefu
Image captionMourinho ataka kuifunza Man United kwa muda mrefu
Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa anataka kusalia katika klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi kwa kuwa anapenda maisha yake na timu hiyo.
Mourinho mwenye umri wa miaka 53, alijiunga na klabu hiyo mwezi Julai, na sasa wako katika nafasi ya sita katika jedwali la ligi baada ya mechi 17.
Mnamo mwezo Oktoba, raia huyo wa Ureno alisema kuwa hoteli anayoishi ni janga wakati ambapo kikosi cha United kilikuwa kikiweka matokeo yasioridhisha.
Najua kwamba ipo siku moja wataleta mkataba mpya, nitatia saini.
Mourinho ameongezea kwamba hatoelekea kufunza nchini China, ijapokuwa amekiri kwamba fedha za China zinavutia kila mtu.
Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar amehusishwa na uhamisho wa Shanghai SIPG, ambapo huenda akalipwa kitita cha pauni 400,000 kwa wiki.
Nataka kusalia katika timu yenye changamoto kubwa ya kujipatia ushindi

No comments:

Post a Comment