Meneja wa Manchester united Jose Mourinho amesifu jitihada za Henrikh Mkhitaryan tangu kujiunga na Old Trafford.
Mkhitaryan, 27, alisaini mkataba wa pauni milioni 26 kutoka Borussia Dortmund lakini aliachwa nje ya uwanja mara kadhaa hadi hivi majuzi.
Lakini katika mechi yake ya tatu, alifunga goli lake la kwanza kwenye ligi ya Europa walipokuwa wakimenyana na Zorya Luhansk ya Ukraine.
"Alifanya bidii sana, na kutumia mbinu tofauti, na sasa tunafahamu kwamba kuna talanta hapa," amesema Mourinho.
Meneja wa Manchester united Jose Mourinho amesifu jitihada za Henrikh Mkhitaryan za uhamisho wake tangu kujiunga na Old TraffordMkhitaryan, alikuwa mchezaji wa akiba kwa United kwenye mechi ya ufunguzi waliopata ushindi dhidi ya Bournemouth, lakini alitolewa baada ya mapumziko walipokuwa katika hatua ya kwanza dhidi ya Manchester City mwezi September, na hakushirikishwa tena katika ligi ya Premia hadi mwishoni mwa mwezi Novemba.
Wakati raia huyo wa Armenian alipokosekana, Mourinho alisema kiungo huyo wa kati, alitaka wakati ili kujifahamisha na michuano ya England, na kumtaka mchezaji bora huyo wa ligi ya Bundesligawa msimu wa 2015-16 'Kufanya bidii zaidi''
''Amekuwa na mawazo imara, Mourinho ameongezea. Ana bidii ya kukabiliana na shida zote, anafanya hivyo katika njia nzuri.
''Alijitahidi kuimarisha mbinu zake, na hivi sasa anacheza vyema katika ligi ya Premia , Europa na EFL, na kumemletea furaha , nimeridhika sana.''
Mbio za Mkhitaryan ziliifanya United kuishinda Ukraine huku shambulizi la mwisho la Zlatan Ibrahimovic likisababisha kuhitimu katika droo ya 32 katika kundi A mbele ya Fenerbahce.
Mourinho aliwapumzisha wachezaji kadhaa ikiwemo mlinda lango David De Gea.
Labda Uefa hajaridhika na labda Uefa sasa hivi huchukua pesa kutoka kwa Zorya , jambo ambalo nafikiria Zorya haistahili, ameongeza Mourinho.
No comments:
Post a Comment