TANGAZO


Thursday, November 17, 2016

WAZIRI PROFESA MBARAWA AZINDUA BODI MPYA YA TRL

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Bodi mpya ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) aliyoizindua leo jijini Dar es Salaam. Wa pili  kulia  ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. John Kondoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti mpya wa bodi ya TRL, Profesa John Kondoro alipozindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa akimwonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, moja ya mabehewa yaliyokarabatiwa na Kampuni hiyo alipotembelea karakana ya reli jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wafanyakazi wa kampuni hiyo  jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wafayakazi wa TRL alipoongea nao jijini Dar es Salaam jana.  Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa.Kulia ni Mwenyekiti ya Bodi ya TRL, Prof. John Kondoro.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), alipoongea nao jana mchana jijiini Dar es Salaam.(Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo)

No comments:

Post a Comment