TANGAZO


Tuesday, November 1, 2016

WASHINDI 16 SUPER NYOTA TIGO FIESTA WATAJWA, FAINALI YA MWISHO KUFANYIKA NOVEMBA 5, 2016 JIJINI DAR ES SALAAM

Mratibu  wa Mradi wa Tamasha la Fiesta 2016 kutokaTigo, Balla Shareeph (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kuwataja  washindi 16 Super Nyota Tigo Dar es Salaam leo. Kulia ni Mratibu wa shindano hilo, Nickson George na katikati ni Mshindi wa shindano, Galla Mligo 'Galla Bway' kutoka Dar es Salaam ambaye alizungumza kwa niaba ya washindi wote.
Mratibu wa shindano hilo, Nickson George (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mshindi wa shindano, Galla Mligo 'Galla Bway' kutoka Dar es Salaam, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Mradi wa Tamasha la Fiesta 2016 kutokaTigo, Balla Shareeph (kushoto) na Mratibu wa shindano hilo, Nickson George kulia wakimkabidhi simu Mshindi wa shindano hilo, Galla Mligo 'Galla Bway' wa Dar es Salaam kwa niaba ya washindi wote ambao walikabidhiwa simu hizo.
Waratibu wa shindano hilo na washindi wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI inayo ongoza kwa maisha ya kidijitali ya TigoTanzania  leo imewatangaza washindi 16 washindano la Tigo Fiesta Super Nyota lililofanyika katika mikoa 15 ya Tanzania Bara. 

Shindano hilo lililoratibiwa na Kampuni ya Prime Time Promotions liliendeshwa katika mikoa hiyo kwa kipindi cha miezi miwili na nusu. 
Mshindi wa fainali yake atajulikana wakati wa fainali ya mwisho Novemba 5, 2016 itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari wakati wa kutangaza washindi hao, Mratibu  wamradi wa Tamasha la Fiesta 2016 kutokaTigo, Balla Shareeph
alisema, “ Tigo inaonafahari kuinyanyua sekta ya muziki ya Tanzania  kwa kuwapatia wasanii wanaoibukia jukwaa la kuonesha vipaji vyao waweze kufikia kiwango cha juu nchini na wakati huo huo kuwawezesha kutambuliwa na chapa mbalimbali za muziki.”

Shareeph aliwapongeza washindi kwa kutumia nafasi hiyo kuwakumbusha wao wenyewe pamoja na umma kwa ujumla kwamba wana weza kupata tiketi zao kwa ajili ya fainali hiyo ya kuhitimisha Msimu wa Fiesta 2016 ambalo litafanyika katika viwanja vya Leaders Novemba 5, 2016  kwa kutumia mtandao waTigoPesa.

Shareeph alifafanua, “Ili kupata tiketi kupitia Tigo Pesa wateja wote wa Tigo na wasio katika mtandao huu wanatakiwa kulipia tiketi kwenda namba 0678 888 888. 

Mkakati huu unalenga kuwapatia watanzania njia ya kawaida na rahisi ya kupata tiketi zao.”  

Washindi Super Nyota 16  ambao ni Nchama Anton a.k.a Nchama, Raphael  Charles  Manengo a.k.a Manengo kutoka (Mwanza), Ibrahim Juma a.k.a Mpanduji (Shinyanga) , Obed  Moses   a.k.a    O strings (Muleba), Salum Asman a.k.a Alinacha ( Kahama), Gasper Festoa.k.a  YOW (Tabora)  Alex Joseph. a.k.a  TIZO ( Singida) na Godfrey Andrew Mhoja a.k.a  NEXUS ( Dodoma).

Wengine ni Hamad Hussein  a.k.a  Med Botion (Morogoro)  Cyril Henry Isidor a.k.a So Real (Tanga) Wilson Pascal     a.k.a  Willy Desmiller( Mtwara )   Charles Mariki a.k.a Gerere (Moshi)  Mohammedy Amiry a.k.a Croozy (Arusha), Amina Chibaba a.k.a Ammy Chiba  (Mbeya) na Leonard John  Haule a.k.a sauti classic (Sumbawanga), watazawadiwa simu ya kisasa yaTecno  Y3+ Music, ikiwa na muda wa maongezi.

Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia  naMratibu washindano la Super Nyota  chini ya mrengo   waMsimuwa Fiesta 2016, Nickson George ambaye alisema, “Tunayo fuhara kubwa kutangaza kwamba washindi 16 Super Nyota ambao watashiriki katika Fainali Kuu ya Fiesta 2016. 

Tunatarajia kuendelea kishukuru jamii kwa kuandaa shindano kama hili katika kuinyanyua sekta ya muziki na burudani ndani ya Tanzania.”

MsimuwaTigo Fiesta 2016   ni tukio linaloendesha kwa ubia baina Kampuni ya Prime Time Promotions naTigo Tanzania na  wakati huo huo Tigo ikiwa ndio mdhamini mkuu.(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)

No comments:

Post a Comment