TANGAZO


Monday, November 7, 2016

SHIRIKISHO LA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU WAPONGEZWA KWA KUWA NA UBUNIFU

Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Utawala ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Kirumbe Ng’enda akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu wa Chama hicho (hawapo pichani) wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Hamid Saleh Mhina na Katibu Msaidizi wa Shirikisho Bw. Daniel Zenda. 
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Hamid Saleh Mhina akizungumza jambo katika wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania ambaye pia kwa sasa anashikiria nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Bw. Daniel Zenda akifafanua jambo wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Imani Matabula na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Taifa, Bw.Hamid Saleh Mhina. 
Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania ambaye pia ndiye alikuwa Mratibu wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ndugu Mgwanwa Nzota akielezea jambo wakati wa Kongamano hilo jana Jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Imani Matabula akizungumza wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Msaidizi wa Shirikisho hilo Taifa, Daniel Zenda, mgeni rasmi katika kongamano hilo ambaye pia ni mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (Mnec) Kirumbe Ng’enda na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Taifa, Hamid Saleh Mhina. 
Mgeni rasmi katika Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bw. Kirumbe Ng’enda akiteta jambo na Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania Bw. Daniel Zenda (kulia) wakati wa kongamano hilo jana Jijini Dar es Salaam. 
Juu na Chini: Baadhi ya wanachama wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania wakichangia mada wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam. 

Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Taifa, Bi. Deborah Charles, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Imani Matabula na Mgeni rasmi (Mnec) Kirumbe Ng’emba wakiandika hoja zilizoibuliwa na washiriki wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli lililofanyika Jijini Dar es Salaam jana. 
Baadhi ya watendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja wanachama wa Shirikisho hilo kutoka vyuo mbalimbali vya Jijini Dar es Salaam baada ya Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli  kumalizika jana Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Mpiga picha wetu)

No comments:

Post a Comment