TANGAZO


Monday, November 28, 2016

Mourinho hatarini ya kuadhibiwa na FA

Jose Mourinho

Image copyrightREUTERS AND GETTY IMAGES
Image captionJose Mourinho alitumikia marufuku ya mechi moja dhidi ya Swansea chini ya mwezi mmoja uliopita
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anakabiliwa na uwezekano wa kuadhibiwa tena na Chama cha Soka Uingereza (FA) baada ya kufukuzwa uwanjani na refa Jumapili.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwake kufukuzwa uwanjani na mwamuzi katika kipindi cha mwezi mmoja.
Mreno huyo alifukuzwa na mwamuzi Jon Moss baada yake kuonekana kukerwa na uamuzi wa refa huyo wa kumuonesha Paul Pogba kadi ya manjano kwa kujiangusha uwanjani mechi ya dhidi ya West Ham, na akapiga chupa teke kwa hasira.
Mechi hiyo ilimalizika sare 1-1.
Video zinaonesha mchezaji wa West Ham Mark Noble hakumgusa Pogba hata kidogo.
Mourinho, pia alifukuzwa uwanjani mwezi uliopita na refa Mark Clattenburg wakati wa mechi iliyomalizika sare 0-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Burnley.
Alitumikia marufuku ya mechi moja wakati wa mechi dhidi ya Swansea.
Katika kisa kingine, alitozwa faini ya £50,000 kwa tamko lake kuhusu mwamuzi Anthony Taylor kabla ya mechi kati ya Manchester United na Liverpool.
Moss pia alimfukuza uwanjani Mourinho Oktoba 2015 Mreno huyo alipokuwa anaikufunza Chelsea wakati wa mechi dhidi ya West Ham.
Mourinho akipiga chupa teke wakati wa mechi dhidi ya West HamImage copyrightREUTERS
Image captionMourinho akipiga chupa teke wakati wa mechi dhidi ya West Ham
Matokeo ya Manchester United baada ya mechi 13 ligini...Meneja
2016-17: alama 20, nambari sitaJose Mourinho
2015-16: alama 27, nambari mbiliLouis van Gaal
2014-15: alama 22, nambari nneLouis van Gaal
2013-14: alama 22, nambari naneDavid Moyes
Man Utd waendelea kudidimia
Mambo yanaendelea kuwa mabaya...
Manchester United sasa wameshindwa kupata ushindi mechi nne za ligi mfululizo Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu Februari 1990
Na pia wametoka sare nyumbani mechi nne mfululizo nyumbani kwa mara ya kwanza tangu Desemba1980.

No comments:

Post a Comment