TANGAZO


Friday, November 11, 2016

RAIS DK. MAGUFULI AONGOZA HAFLA YA KUUAGAJI MWILI WA MAREHEMU MHE. SAMWEL SITTA KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM

Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta Ukiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.(Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.  
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.  
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.  
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko, pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli(Katikati), Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye shungi), Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa (wa mwisho kushoto) na Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif alli Idd (wa mwisho kulia) wakifuatilia idaba ya kuuaga Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta katika viwanja vya Karimjee kwa ajili.  
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta ukiwa katika eneo maalum mbele ya waombolezaji kwa ajili ya kufanyiwa idaba na tukio la utoaji heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi Mhe. Angela Kairuki akitoa salamu za serikali wakati wa shughuli ya utoaji heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwaeleza jambo Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Alli Idd (katikati) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisalimiana na wafiwa wakati wa shughuli za utoaji heshima kwa mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta. 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko. 
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Viongozi wastaafu wakiwapa pole ndugu na waombolezaji wakati wa shughuli za utoaji heshima kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta. 
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Viongozi wastaafu wakiwapa pole ndugu na waombolezaji wakati wa shughuli za utoaji heshima kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta. 
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Sinde Warioba, akimpa pole mke wa marehemu, Mama Magreth Sitta, wakati wa shughuli za utoaji heshima kwa mwili wa marehemu Spika mstaafu, Mhe. Samwel Sitta. 
Baadhi ya viongozi na waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.

Frank  Mvungi, Maelezo, Dar es Salaam.
11.11.2016.
RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaongoza mamia ya Watanzania ikiwemo Viongozi wa Chama na Serikali kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Spika Mstaafu Marehemu Samweli Sitta katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Akiwasilisilisha Salamu za Serikali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Mhe. Angellah Kairuki amesema Serikali imempoteza Kiongozi mwadilifu, mzalendo na mchapa kazi ambaye wakati wote alifanya kazi kwa maslahi ya nchi yake.

Aidha amesema  Taifa limempoteza mtu mnyenyekevu, mwanamapinduzi na mpenda haki aliyejitoa kuwatumikia watanzania kwa takribani miaka 49 ya utumishi wake Serikalini.

Kwa upande wake, Jaji Kiongozi Ferdnand Wambali amesema kuwa Taifa limempoteza mtu Jasiri aliyetetea wanyonge wakati wote na kuishi maisha ya uadilifu.

“Marehemu Sitta aliwahi kuitwa na mahakama ili kutoa ushahidi kwenye kesi ya ajali za barabarani na aliwahi mahakamani siku husika hata kabla ya shughuli za mahakama kuanza saa moja asubuhi yeye alikuwa ameshafika hii ilionyesha unyenyekevu wake” Alisisitiza Jaji Kiongozi  Wambali.

Jaji Kiongozi Wambali ameongeza kuwa wakati wote Marehemu Mhe. Sitta alijitoa kutoa ushauri kila alipohitajika bila kusita na kusimamia kile anachokiamini.

Kwa Upande wake Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mchungaji Chediel Luiza amesema Mhe. Marehemu Sitta alikuwa Kiongozi na mtumishi wa watu katika kipindi chote cha uhai wake.

Aliwataka watu wote kuwatumikia watu wasio na uwezo na uadilifu na upendo ili kutimiza yale yawapasayo kufanya kama Mwenyezi Mungu anavyoelekeza kwa ustawi wa Taifa letu.


Spika mstaafu Samweli Sitta ameshika nyadhifa mbalimbali Serikalini zikiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Uwaziri, Mkuu wa Mkoa,Mkurugenzi wa Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC).

No comments:

Post a Comment