TANGAZO


Wednesday, November 2, 2016

Guardiola: ushindi dhidi ya Barcelona ni mafanikio makubwa

Guardiola anasema Man City walicheza kwa njia isiyo ya kawaida

Image copyrightREUTERS
Image captionGuardiola anasema Man City walicheza kwa njia isiyo ya kawaida
Meneja wa Manchester City Pep Gurdiola anasema ushindi wa klabu hiyo wa mabao 3-1 dhidi ya Barcelona na ushinidi mkubwa kwa klabu yake.
Manchester City hawajawai kuwashinda Barcelona kwenye mechi tano ambazo zimepita na Guardiola anasema kuwa ni jambo lili zuri kusema kuwa kwa mara ya kwanza wamecheza na klabu bora zaidi duniani na kuwashinda.
"Tumeshindana na Barcelona, lakini kwa sasa tumefanya kwa njia tofauti. Tulicheza mipira mirefu kwa sababu hatuko tayari kucheza jinsi wanavyocheza." alisema Guardiola.
Guardiola alishinda kombe mara mbili akiwa na Barcelona mwaka 2009 na 2011Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionGuardiola alishinda kombe mara mbili akiwa na Barcelona mwaka 2009 na 2011
Ushindi wa Man City unaweka katika nafasi ya pili kwenye jedwali nyuma ya Barcelona ikiwa sasa inahitaji ushindi mmoja zaidi kutoka kwa mechi mbili zilizosalia kuweza kusonga mbele kwa kundi la timu 16 bora.
Guardiola ambaye alishinda kombe mara mbili akiwa Meneja wa Barcelona, alipata kipigo wakati Man City ilishindwa kwa mabao 4-0 uwanja wa Nou Camp mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment