Fundi wa Kivuko cha Mv Chato kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Bw. Mbondo Jackson, akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, namna injini ya Kivuko cha MV. Chato inavyotumia mafuta, alipotembelea kivuko hicho, wilayani Chato, Geita.
Muonekano wa Kivuko cha MV Chato kilichopo Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye shati la blue), ramani inayoonesha mtandao wa barabara za mkoa wa Geita, alipomtembelea Ofisini kwake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (hawapo pichani), alipoongea nao Mkoani Geita.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisalimiana na wafanyakazi wa
Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mara baada ya kuongea nao Mkoani
Geita.
SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), imeanzisha Kitengo maalum cha
Wahandisi Washauri (TECU), ili kuwajengea uwezo wahandisi wazawa kusimamia miradi
ya ujenzi wa barabara nchini na hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha
ambacho kingetumika kuwalipa wahandisi washauri kutoka nje ya nchi.
Akizungumza
mkoani Geita mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya
Uyovu-Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 112 ambayo pia inasimamiwa na Wahandisi
Washauri Wazawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
amesema mpaka sasa wahandisi wazawa wanasimamia miradi mbalimbali ya barabara
katika mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita na Kilimanjaro ambapo kupitia miradi hiyo
serikali imeokoa dola za kimerani milioni mbili ambazo zingetumika kulipa
wahadisi kutoka nje ya nchi.
"Nitahakikisha ninakijengea uwezo
kitengo hiki ili kuweza kuokoa fedha nyingi zaidi. Nimeridhishwa na usimamizi
wa wahandisi hawa katika barabara hii ambayo ipo katika hatua nzuri",
amesema Prof Mbarawa.
Waziri
Mbarawa ameongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa miaka mitano ijayo miradi
yote mikubwa nchini itasimamiwa na Wakala huo ili kuokoa fedha za ndani na
badala yake fedha hizo kuelekezwa kwenye miradi mingine ya ujenzi.
Kwa
upande wake, Meneja wa TANROADS, mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku amesema kuwa mradi wa ujenzi wa
barabara ya Uyovu-Bwanga umefikia asilimia 47 na Bwanga - Biharamulo
umefikia asilimia 42 na ujenzi wake unagharimu
zaidi ya shilingi Bilioni 90.
Aidha,
Eng. Senkuku amemuahidi Waziri huyo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili
wananchi wa mikoa ya kagera na Geita kuweza kutumia barabara hiyo.
Naye,
Mhandisi Msahauri kutoka TECU Eng. Gladson Yohana amesema kuwa kusimamia miradi
mikubwa kama hiyo kumewasaidia kujifunza zaidi kwa vitendo na amemuhakikishia
Waziri huyo kusimamia barabara hiyo kwa kuzingatia ubora na viwango
vinavyotakiwa.
Katika
hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua kivuko cha MV. Chato na kumuagiza
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), mkoa wa Geita Eng.
Fredinand Mishamo kuhakikisha kuwa kivuko hicho kinajiendesha chenyewe
kutoka kwenye mapato yanayopatikana.
Prof
Mbarawa amemtaka Meneja huyo kuhakikisha kuwa mapato yatokanayo na kivuko hicho
yanaongezeka ili kuweza kusaidia changamoto ndogondogo katika kivuko hicho.
Eng.Mishamo amemuelezea Waziri huyo
changamoto zinazokabili kivuko hicho kuwa ni kukosa maegesho katika baadhi ya
maeneo.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment