Sehemu ya wakazi wa Nankanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani) wakati wa Waziri akiwahimiza juu ya kutuza rasilimali za Mazingira.
Mifugo ikichungwa pembezoni mwa Ziwa Rukwa Waziri Makamba amegiza shughuli za aina hiyo kufanyika mita 200 kutoka kwenye chanzo cha maji.
Sehemu ya Viongozi
wa dini, siasa na wazee wa Mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Muungano
na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani), alipokutana nao na kusisitiza amani na Hifadhi ya mazingira.
Na
Lulu Mussa, Sumbawanga
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameendelea na ziara
ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara yake siku ya leo Waziri Makamba
ameshuhudia uharibifu mkubwa wa mazingira hususan pembezoni mwa ziwa Rukwa.
Waziri Makamba
amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha
Nankanga kwamba mwaka 2000 kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita
sita, na kwa mwaka 2016 chanzo hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu.
"Tafiti zinaonyesha kuwa kupungua kwa kina hicho pamoja na mambo
mengine kunasababishwa na kilimo cha
milimani na kandokando ya ziwa, na ulishaji wa mifugo katika Vyanzo vya
maji" Makamba alibainisha.
Katika ziara yake baada ya
kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri Makamba ameazimia kulitangaza
eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa mazingira na kanuni za matumizi ya
maeno hayo zitaandaliwa ili kunusuru Ziwa Rukwa.
Pia, wakurugenzi wote wa
Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga pesa zitokanazo na tozo
mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa alama maalum 'beacons' ili kuainisha
eneo tengefu na kuagiza kuwa zoezi hili lifanyike haraka.
Aidha, Mhe. Makamba
amesisitiza juu ya upandaji wa miti na ameonyesha masikitiko yake kwa Mkoa wa
Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili na ile ya kupanda kwa kiwango kikubwa.
"nimetembea zaidi ya kilomita 200 sijaona miti iliyopandwa" Makamba
aliongezea.
Wakazi wa Mkoa wa Rukwa wamefahamishwa
na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani itakuwa lazima kwa wanafunzi wa Primary na
Sekondari kuwasili na miti na kutakiwa kuitunza mpaka pale watakapomaliza
shule. Waziri Makamba ameahidi kuleta wataalamu na kutoa orodha ya miche
inayostawi katika kila kijiiji ili kurahisisha uoteshaji wa miti.
Katika hatua nyingine,
Waziri Makamba amekutana na viongozi mbalimbali za dini na wazee wa Mkoa wa
Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani, na kuahidi kugharimia Mkutano wa
kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo na kusisitiza agenda ya Mazingira iwepo.
Mkoani Rukwa Waziri Makamba
ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo na
Mkutano wa Hadhara katika Kijiji cha Nankanga ambapo wakazi wa maeneo hayo
wamempongeza kwakua toka kijiji hicho kianzishwe mwaka 1974, Waziri Makamba
ndio amekuwa mgeni wa kwanza Kitaifa kuwatembele.

No comments:
Post a Comment