Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach, (Bunju Beach Community Support), Bi. Vanessa Milinga akisoma risala ya Jumuiya hiyo wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach (Bunju Beach Community Support), Bi. Vanessa Milinga mara baada ya kumkabidhi risala wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
Muasisi wa Jumuiya ya Bunju Community Support Profesa. Joas Rugemalila (kushoto) akigonga cheers na RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
RPC
wa Kinondoni Suzan Kaganda wakigonga cheers
wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini
Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
(Picha zote na
Mpigapicha wetu)
Na Mwandishi Wetu.
SUALA
la wizi na ujambazi kwa wakazi wa Bunju Beach kubakia kuwa historia baada ya
Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni kuahidi kujenga kituo cha Polisi
kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua Askari zaidi ya 40.
Hayo
yamebainishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzan Kaganda
alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua umoja wa Wakazi wa Bunju “Bunju Beach Community Support.”
RPC
Kaganda amesema kuwa wezi na majambazi wamekula kwao na kuongeza kuwa suala la
ulinzi na usalama ni la kila raia kwa mujibu wa sheria.
Awali
akisoma risala ya Jumuiya hiyo Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya kusaidiana ya
Wakazi wa Bunju (Bunju Beach Community Support),
Vanessa Milinga alisema kuwa Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na lengo
la kuimarisha ulinzi na usalama wa mali na familia za wakazi wa Bunju Beach.
Vanessa
amesema kuwa mwaka 2011 walipata usajili ambapo pia wanachama wameongezeka na
kupelekea kubadili kuongezeka kwa malengo ambayo ni pamoja na kuanzishwa kwa
SACCOSS.
Akizungumzia
historia ya Bunju Beach Community Support,
Mmoja wa waanzilishi wa Jumuiya hiyo Profesa. Joas Rugemalila amesema kuwa
umoja huo umeanzishwa kwa lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi, usalama, amani
na maendeleo.






No comments:
Post a Comment