TANGAZO


Monday, October 10, 2016

Raia wa Malawi wataka rais wao arudi nyumbani

Rais Mutharika aliondoka Malawi wiki mbili zilizopita na hadi sasa hajarudi

Image copyrightREUTERS
Image captionRais Mutharika aliondoka Malawi wiki mbili zilizopita na hadi sasa hajarudi
Serikali ya Malawi imekanusha ripoti kuwa Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika yuko mgonjwa sana nchini Marekani.
Raia wa Malawi kwenye mitandao ya kijamii wanatumia #BringBackMutharika, wakitaka Rais wao arudi nyumbani baada ya kuondoka nchini humo wiki mbili zilizopita kuhudhuria mkutano wa umoja wa mataifa mjini New York.
Serikali ilisema kuwa bwana Mutharika yuko na afya nzuri na alikuwa akikamilisha shughuli za serikali ambazo hakuwa na muda wa kuzishughulikia akiwa kwenye Umoja wa Mataifa,
Ukurasa wa serikali kwenye mtandao wa Facebook ulisema kuwa tarehe itatangwazwa ya kurudi kwa rais nchini Malawi.

No comments:

Post a Comment