Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Kampuni ya Songoro wanaojenga kivuko kipya cha MV. Kazi, kinachojengwa katika yadi ya Bandari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutembelea na kujionea ujenzi wake.Kivuko hicho kipya kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa akiongea na mafundi wa wa Kampuni ya Songoro wanaojenga kivuko kipya cha MV. Kazi, kinachojengwa katika yadi ya Bandari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutembelea na kujionea ujenzi wake.Kivuko hicho kipya kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), alipotembelea eneo la Kivukoni. Katikati ni Mkuu wa Kivuko upande wa Dar es Salaam, Eng. Lukombe King’ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiongea na mwanafunzi Arafat Kondo wakati alipotembelea kivuko cha MV. Kigamboni kujionea utendaji wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akishuka kwenye pantoni mara baada ya kukagua utendaji wa kivuko cha MV. Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisikiliza taarifa ya matumizi
ya mafuta kutoka kwa Mhandisi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) alipotembelea kivuko cha MV.
Kigamboni.
WAZIRI wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameuagiza uongozi wa Wakala wa
Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ya
kuongeza mapato katika vivuko vya MV. Kigamboni na MV. Magogoni kutoka Shilingi
Milioni 14 ambazo zinakusanywa hivi sasa hadi kufikia Milioni 19 kwa siku.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam mara baada ya kukagua vivuko hivyo na kuongea na Mtendaji Mkuu wa
TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu Prof. Mbarawa amesema kuwa kipimo cha utendaji huo
utafanyika ndani ya miezi minne ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa
vivuko hivyo na kuweza kufikia malengo.
“Hatushindwi kutafuta
mtu mwingine mwenye ujuzi na utendaji wa kazi uliotukuka, kama lengo la
kukusanya milioni 19 halitafikiwa mkuu wa kivuko atafute kazi nyingine na tutafanya hivyo mpaka tuhakikishe tunapata
atayeweza kukusanya kiwango hiki”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa ameutaka
Wakala huo kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato katika vivuko hivyo na kuwa
wa kieletroniki ili kudhibiti ubadhilifu unaofanywa na watumishi wasio
waaminifu wakati wa utoaji huduma.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amejionea
maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV. Kazi nakusema kuwa kivuko hicho kitarahisisha
usafiri kwa wakazi wa Kigamboni.
Aidha, amemtaka
mkandarasi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport kumaliza utengenezaji wa
kivuko hicho ifikapo Mwezi Disemba mwaka huu ili watanzania wapate huduma bora
za usafiri.
Ameongeza kuwa Kampuni
hiyo ihakikishe kuwa inasimamia upatikanaji wa injini za Kivuko hicho kwa
wakati ili kusaidia ujenzi huo kukamilika kwa muda uliopangwa.
“Nina imani na kasi
mnayokwenda nayo, na nina uhakika Kivuko hiki kitamalizika kwa wakati naomba
muwe waangalifu na kuhakikisha kwamba injini za kivuko hiki zinawasili mapema”,
amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye Mkurugenzi wa
Karakana ya Dar es Salaam wa Kampuni ya Songoro Marine, Major Saleh Songoro
amesema kuwa ujenzi wa Kivuko cha MV Kazi upo katika hatua nzuri ambapo kwa
sasa wanakamilisha kazi ya kuchomea milango katika kivuko hicho.
Kwa upande wake
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mgwatu amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa maagizo
yote yatatekelezwa ikiwemo kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili Wakala
huo.
Dkt. Mgwatu amewataka
wananchi kuwa na subira wakati kivuko cha MV. Kazi kinamalizika kujengwa kwani
itapunguza kama sio kuondoa msongamano uliopo sasa katika maeneo ya Magogoni na
Kigamboni.
Ujenzi wa kivuko cha
MV Kazi ulianza Mwezi Juni mwaka huu ambapo kina uwezo wa kubeba tani 170 sawa
na watu 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano
No comments:
Post a Comment