TANGAZO


Thursday, October 13, 2016

NAIBU WAZIRI DK. POSSI: ULEMAVU NA UZEE SIO LAANA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa  taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Eleuteri Mangi-Maelezo) 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa  taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es Salaam. 
Wageni waalikwa wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi wakati wa uzinduzi wa  taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es Salaam. 
Wageni waalikwa wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi wakati wa uzinduzi wa  taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es Salaam. 
Wageni waalikwa wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi wakati wa uzinduzi wa  taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es Salaam. 
Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) Bakar Fakih akiwasilisha taarifa ya utafiti waliofanya kuhusu maisha ya wazee na watu wenye ulemavu ambao umebainisha kuwa bado kuna imani potofu kwenye jamii juu ya wazee na watu wenye ulemavu. 
Mshiriki Rika (kundi la wazee) Bi. Elizabeth Nkwera akichangia juu ya utafiti waliofanya wakati wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum walipowasilisha matokeo ya tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini. 
Mshauri Maendeleo ya kijamii kutoka Uingereza Idara ya Maendeleo ya Kimataifa Isabelle Abbott Pugh akitoa mchango wake kuhusu dhana ya kuwajali watu wenye ulemavu na wazee wakati wa uzinduzi wa  taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi akisalimiana  na wazee mara baada ya uzinduzi  wa  taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Bi. Clotilda Isdori Kokupima kutoka wilaya yak ASULU mkoani Kigoma na katikati ni Bw. Elisha Sibale kutoka halamashauri ya Kibaha mkoani Pwani. 
Wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi mara baada ya uzinduzi wa utafiti Mpya wa Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini.

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO
WATAFITI wa masuala mbalimbali ya kijamii nchini wametakiwa kuhakikisha wanafanya tafiti ambazo zitawasaidia watu wenye ulemavu kupata vifaa saidizi ili waweze kumudu kuendesha maisha yao ya kila siku.


Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Possi Abdallah alipokuwa akizindua taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es salaam.

“Serikali inafarijika inapoona watu wanafanya utafiti ili kuwasaidia watu wenye ulemavu waweze kupata vifaa saidizi na ni kitu gani kifanyike ili NGOs ziweze kujikwamua kiuchumi na kuwasaidia wenye mahitaji” alisema Dkt. Possi.

Kuhusu suala la unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu, Dkt. Possi amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu hapo tayari kuona wananchi wananyanyapaliwa huku akisisitiza kuwa watu wote ni sawa na ofisi hiyo ina “zero tolerance” kwa watu wanaowanyayapaa mlemavu.

Katika masuala ya kisheria kwa watu wenye ulemavu, Dkt. Possi amesema kuwa inapotokea mlemavu au mzee amefanyiwa kosa taarifa itolewe mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya waliofanya makosa hayo na haki iweze kutendeka.

Naibu Waziri Dkt. Possi pia amezitaka Asasi zinazoshughulika na watu walemavu wafanye kazi kwa pamoja ili kuwasaidia walengwa ambao ni walemavu, watoto na wazee na kuwataka kutumia fursa waliyonayo ya kupata msaada kisheria bure kutoka kwenye taasisi za sheria ikiwemo Chama cha Mawakili (Tanganyika Law Society), TAMWA pamoja na  taasisi nyingine za kisheria wakati masuala ya jianai amewataka wayapeleke kwenye polisi kwa hatua zaidi za kisheria huku akisisitiza kumshirikisha inapobidi kufanya hivyo.

Akitoa maelezo ya utafiti huo wakati wa uzinduzi, mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) Bakar Fakih amesema kuwa utafiti huo umewashirikisha watafiti rika mbalimbali wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu na kubainisha kuwa bado kuna imani potofu kwenye jamii juu ya wazee na watu wenye ulemavu.

Utafiti huo unaoongozwa na kaulimbiu “Ulemavu na uzee sio laana” umebainisha kuwa watu wenye ulemavu na wazee nchini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata elimu, huduma za afya, unayanyasaji wa kingono na kuvunjika kwa ndoa, kutokujaliwa na familia pamoja na kutengwa kwa watu wenye ualbino kutokana na mila potofu.

Kwa upande wake mtafiti rika Blandina Isaya amesema kuwa walemavu waachwe wafanye maamuzi yanayohusu maisha yao ikiwemo masuala ya ndoa wawe huru kuchagua wenza wao badala ya kuchaguliwa na familia zao kwa kuwa wanahaki kama watu wengine wasio na ulemavu.


Katika kuhakikisha familia zinakuwa imara kiuchumi, Blandina amesema kuwa familia zenye watu wenye ulemavu na wazee wapewe elimu ya ujasiriamali ili waweze kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yao kwa kulea familia ipasavyo na kuomba Seriklai za mtaa ziwe na takwimu za wazee na watu wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment