TANGAZO


Saturday, October 8, 2016

NAIBU MAWAZIRI WA OFISI YA WAZIRI MKUU WATEMBELEA BANDA LA MAONESHO LA ELIMU YA MPIGA KURA LA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) LEO WILAYANI BARIADI MKOANI SIMIYU

Afisa Habari wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Margareth Chambiri (kulia) akiwakaribisha kwenye banda la Maonesho la NEC, Naibu Mawaziri Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea na program endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura kote nchini.
Naibu Mawaziri Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakipata ufafanuzi kutoka kwa Maafisa wa NEC kuhusu utendaji wa Mashine za BVR katika uchukuaji na uhifadhi wa taarifa za Wapiga Kura leo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi –Simiyu.
Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Sanif Khalifan akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bariadi kuhusu taratibu za uchaguzi na hatua za uandikishaji wa wapiga kura kupitia TEHAMA leo mjini Baridi wakati wa Tume hiyo ilipokuwa ikitoa Elimu kwa Mpiga Kura kuhusu masuala mbalimbali.
Baadhi ya Askari wa JKT wakipita mbele ya Banda la Maonesho la NEC na wengine wakipata ufafanuzi kuhusu masula mbalimbali walipotembelea Banda la Maonesho ya Elimu ya Mpiga Kura wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.

Naibu Mawaziri Mhe. Anthony Mavunde - Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakifurahia jambo mara baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwa Maafisa wa NEC kuhusu utendaji wa Mashine za BVR katika uchukuaji na uhifadhi wa taarifa za Wapiga Kura leo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi –Simiyu.
Mkazi wa Bariadi akipata ufafanuzi kuhusu karatasi zenye majina ya wagombea zinazotumika kupigia kura alipotembelea banda la maonesho na Elimu ya mpiga kura la NEC leo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.(Picha zote na Aron Msigwa – NEC)

No comments:

Post a Comment