TANGAZO


Saturday, October 15, 2016

Maafikiano kuhusu gesi joto duniani wapatikana Rwanda

John Kerry

Image captionWaziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry aliwahimiza washiriki kuafikiana
Maafisa nchi zaidi ya 150 ambao wamekuwa wakikutana nchini Rwanda wameafikiana mkataba muhimu wa kumaliza hatua kwa hatua gesi ambazo zimekuwa zikichangia ongezeko la joto duniani.
Gesi hizo kwa Kiingereza Hydroflurocarbons (HFCs) hutumiwa sana katika jokofu, viyoyozi na dawa za kunyunyiziwa zenye aerosol.
Wajumbe waliokuwa wamekutana Rwanda walikubaliana kuhusu marekebisho kwenye Mkataba wa Montreal ambao utapelekea nchi tajiri kupunguza matumizi yake ya HFC kuanzia 2019.
Baadhi ya wakosoaji wa mkataba huo wanasema matokeo ya mkataba ulivyo sasa hayatakuwa kama ilivyotarajiwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, aliyesaidia sana kuwashawishi wajumbe waunge mkono mktaba huo, alisema maafikiano hayo ni ushindi mkubwa kwa dunia.
Chini ya mkataba huo, kutakuwa na nja tatu kuu kwa mataifa mbalimbali.
Mataifa tajiri ya Umoja wa Ulaya, Marekani na mataifa mengine kadha yatapunguza matumizi yake ya HFC katika kipindi cha miaka michache ijayo na kuhakikisha wamepunguza kwa angalau 10% kuanzia 2019.
Nchi kadha zinazoendelea kama vile Uchina na nchi za Amerika Kusini pamoja na mataifa mengine ya visiwani, zitasitisha matumizi ya HFC kuanzia 2024.
Nchi nyingine zinazoendelea, hasa India, Pakistan, Iran, Iraq na mataifa ya Ghuba yatachukua hatua mwaka 2028 na kusitisha matumizi ya HFC.
Kwa China, mzalishani mkuu wa HFC duniani, inatarajiwa kuanza kupunguza uzalishaji wake wa HFC 2029.
Kiyoyozi
Image captionViyoyozi vilihitajika ukumbi wa mkutano Kigali baada ya mazungumzo kuendelea hadi usiku
India, itaanza baadaye kidogo, ikipunguza kwa 10% mwaka 2032.
frijiImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionJokofu mpya au friji sasa zitahitajika kutumia gesi zisizochangia sana ongezeko la joto duniani siku za baadaye

No comments:

Post a Comment