TANGAZO


Sunday, October 9, 2016

Kundi la IS lapoteza robo ya maeneo inayodhibti

Wapiganaji wa Islamic State

Image captionWapiganaji wa Islamic State
Utafiti uliofanywa na kundi moja la wachanganuzi kuhusu ulinzi unasema kuwa kundi la wapiganaji la Islamic State limepoteza zaidi ya robo ya eneo ililokuwa ikidhibiti.
Ripoti hiyo inasema kuwa eneo hilo limepungua kwa asilimia 28 tangu kundi hilo lianze kushambulia na kudhibiti maeneo hayo mwaka 2015.
Kundi hilo sasa linadaiwa kudhibiti eneo lenye ukubwa wa taifa la Siri-Lanka pekee.
Wapiganaji wa Islamic state wamekuwa wakikabiliwa kutoka pande zoteImage copyrightAFP
Image captionWapiganaji wa Islamic state wamekuwa wakikabiliwa kutoka pande zote
Wachanguzi hao wanasema ijapokuwa kasi hiyo ya kupoteza maeneo inayodhibiti imepungua miezi mitatu kabla ya mwezi wa Oktoba,maeneo hayo ni pamoja maeneo muhimu karibu na mpaka na Uturuki,mji wa Syria wa Manbij na kambi moja ya jeshi la angani kusini mwa mji wa Mosul nchini Iraq.

No comments:

Post a Comment