TANGAZO


Monday, October 17, 2016

KIONGOZI WA BOHORA DKT. SYEDNA MUFADDAL SAIFUDDIN AMKABIDHI MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAM, PAUL MAKONDA BAJAJI 2 KWA NIABA YA SAIDI MRISHO ALIYE TOBOLEWA MACHO

Said Mrisho akishukuru kwa wote wanaojitokeza kumpigania kwa hali na mali, hasa akianza na kumshukuru Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwa na maono ya kumchaguwa Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye anauchungu wa wananchi wake na pia akamshukuru Kiongozi wa Mabohora kwa kumsaidia Bajaji 2. 

"Sina cha kuwalipa hawa, ila Mungu atawalipa", alisema Mrisho wakati wa hafla ya kukabidhiwa bajaji 2 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, msaada uliotolewa na Kiongozi wa Mabohora  maeneo ya Upanga, Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa Paul  Pakonda (kushoto), akisalimiana na Kiongozi wa Mabohora, Syedna Dk. Mufaddal Saifuddin (wa tatu kushoto), wakati wa hafla ya kumkabidhi Bajaj 2, Said Mrisho ambaye alietobolewa macho na mtuhumiwa Salum Njewele (Scopion).

Kiongozi wa Mabohora, Syedna Dk. Mufaddal Saifuddin, akipeana mikono na Said Mrisho ambaye alipata upofu wa macho kutokana na kutobolewa na mtuhumiwa Salum Njewele (Scopion), wakati wa hafla ya  kumkabidhi Bajaj mbili, jijini Da es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Said Mrisho (kushoto), akikabidhiwa kadi za Bajaj na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla hiyo. (Picha zote na Khamisi Mussa)

No comments:

Post a Comment