TANGAZO


Monday, October 31, 2016

KAMPUNI YA BAYPORT YASHEREHEKEA MIAKA 10 YA KUANZISHWA KWAKE PAMOJA NA WATOTO WA KCVC

Mgeni rasmi, Mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa, akiongea na wafanyakazi  wa Bayport, waandishi  wa  habari   na  walimu  wa  kituo cha kulelea   watoto   yatima  cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wakati  wakusherehekea    miaka 10 ya Bayport ambayo   ilifanyika  katika  kituo  hicho   juzi, Kibaha  mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mtendaji   wa Bayport, John Mbaga, akiongea na  wafanyakaziwa Bayport, waandishi  wa habari na walimu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wakati wa kusherehekea miaka 10 ya Bayport ambayo ilifanyika katika kituo hicho juzi, Kibaha mkoani Pwani.

Baadhi ya  wafanyakazi  wa Kampuni ya Bayport Tanzania wakiwavalisha fulana watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulelea  Watoto Yatima cha Kibaha Children Village Center, wakati  wafanyakazi hao walipokwenda   kusherehekea miaka 10 ya kampuni hiyo.

Wafanyakazi   wa Bayport wakipiga   picha  ya   pamoja   kwenye   bango  lao.

Watoto wakibembea wakati wa kusherehekea miaka 10 ya Bayport Tanzania.

Watoto  wakiwa wanakula pamoja kusherehekea miaka 10 ya Bayport Tanzania.














Wafanyakazi wa  bayport wakiwa  katika  picha  ya pamoja  na viongozi, watoto yatima na watoto wa wafanyakazi wa Bayport Tanzania, wakati wa kusherehekea miaka 10 ya Bayport ambayo ilifanyika   katika kituo cha kulelea   watoto  yatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wengine  pichani (kulia kwa Mama Mkapa) ni   Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport John Mbagana  Mkuu  wa  kitengo cha Masoko   na Mawasiliano  Ngula Cheyo.

No comments:

Post a Comment