TANGAZO


Wednesday, October 12, 2016

8 wauawa katika maandamano ya Ashura Nigeria

Waumini wa madhehebu ya Shia wamekuwa wakiandamana siku ya Ashura

Image copyrightALI KAKAKI
Watu wanane wameuawa katika mapigano kati ya vikosi vya usalama Nigeria na waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji wa kaskazini wa Funtuna, shahidi mmoja ameiambia idhaa ya Hausa ya BBC.
Mauaji hayo yametokea baada ya jeshi na polisi kuzuia maandamano ya kila mwaka ya madhehebu hayo katika kuadhimisha Ashura - siku ya kumbukumbu ya mjukuu wa mtume Muhammad - Hussein kutawazwa kuwa Shujaa, aliyekufa shahidi.
Risasi zilifyetuliwa na kusikika kila mahali, jamaa mmoja aliyeshuhudia ghasia hizo amesema.
Ameongeza kuwa alihesabu miili 8 ya watu huku wengine zaidi wanahofiwa kujeruhiwa.
Jimbo la Katsina, kama ilivyo kwa majimbo mengine kaskazini mwa Nigeria, yamepinga maandamano ya leo ya madhehebu ya Shia.

No comments:

Post a Comment