Na
Ally Daud, Maelezo
Dar
es Salaam
7.9.2016
HOSPITALI za Muhimbili, Amana, Mwananyamala na Kairuki za Jijini Dar es Salaam zinatarajia
kuwekwa kwenye mradi maalum wa kudhibiti taka hatarishi ikiwa ni mkakati wa
Serikali wa kuboresha usafi wa mazingira katika huduma za afya nchini.
Mradi huo wa
kudhibiti taka
hatarishi ikiwemo sindano, gloves, nyembe na bandeji unasimamiwa na Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mazingira
uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma ya Afya na Kinga
kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Neema Rusibawengile
alisema kuwa lengo la mradi huo una
lengo la kukabiliana na magonjwa ya maambukizi katika maeneo ya hospitali
nchini.
“Mkutano
huu umelenga kuandaa na mradi
utaodhibiti taka hatarishi amabao utanza kufanya kazi katika hospitali za
Muhimbili,Amana,Mwananyamala kairuki na baadaye kuendelea nchi nzima” alisema
Dkt Rusibawengile.
Dkt. Rusibawengile
alisema kuwa mkutano huo pia
umewakutanisha wadau mbalimbali wa Maendeleo na Mazingira watakaojadili mbinu
mpya za kutunza mazingira kwa ajili ya kupeuka magonjwa ya maambukizi nchini
yanayotokana na taka hatarishi.
Kwa mujibu wa Dkt
Rusibawengile alisema mkutano pia huo
unalenga kupata njia mbadala za kupunguza uzalishaji wa mekyuri katika
hospitali, zahanati na vituo vya afya ili kuondoa utumiaji wa vifaa vyenye nishati
hiyo.
Kwa upande wa mratibu
wa udhibiti wa taka hatarishi za Hospitali Dkt. Honest Anicetus alisema wadau wa mkutano huo pia wamepanga kubuni
mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya afya katika utunzaji wa mazingira.


No comments:
Post a Comment