Mkurugenzi Mtendaji
kampuni ya Heritage Rukwa Tanzania
Limited Bw Jim Baban akichangia jambo wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya
shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.Kulia kwake ni Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Dorsal Bw. P.K Surendran.
(Picha zote na Daudi Manongi-Maelezo) Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Dorsal Bw,P.K Surendran na wa pili kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Heritage Rukwa Tanzania Limited.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Dorsal Bw. P.K Surendran akizungumza kuhusu hatua iliyofikiwa ya shughuli za utafutaji wa mafuta na Gesi.Kushoto kwa Mkurugenzi uyo ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi mtendaji Heritage Rukwa Tanzania Limited Bw Jim Baban(wa tatu kushoto),Meneja Mkazi wa shirika la Statoil Tanzania фystein Michelsen na Kaimu kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petrol nchini Bw.James Andilile.
Wadau wa Gesi na Mafuta wakimskiliza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw.Kapulya Msomba akieleza maendeleo ya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi yaliyofikiwa na shirika hilo kwa wadau wa Mafuta na Gesi jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Kaimu kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petrol nchini Bw.James Andilile na Meneja Mkazi wa shirika la Statoil Tanzania Bw. фystein Michelsen.
Kaimu kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli nchini Bw.James Andilile akijadili na wadau wa mafuta na gesi shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini. Kushoto kwake Meneja Mkazi wa shirika la Statoil Tanzania фystein Michelsen.







No comments:
Post a Comment