Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya ambao walitoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Septemba 22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini .Kutoka kushoto ni Sheikh Tahir Mahmood Chaundhry, Issa Mwakitalima, Khuram Shahzad na Jamil Mwanga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw. Ian Ferrao (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ukiwa ni mchango kwa waarhirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa Meneja wa Kanda wa LAPF, Amina Kassim (kulia) na Kafiti Kafiti wa LAPF ukiwa ni mchango wa Mfuko huo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea sehemu ya msaada ya vyakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa viongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Art of Living ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Kutoka kushoto ni Nishitha Kulshreshtha, Nishit Patel, Neha Movaliya,Sharik Choughule ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Shina la Pamba Road, Upanga na Neha Movaliaya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa tani 40 za saruji zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 kutoka kwa Dhruv Jog na Lebulu Victor (kulia) wote wa Kampuni ya ujenzi a Advent ukiwa ni mchango kwa waahirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza kiongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Art of Living Nishitha Kulshreshtha, baada ya kupokea msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kutoka kwa viongozi wa Mfuko huo Jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Neha Movaliaya, Sharik Choughule ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Shina la Pamba Road, Upanga, Nishit Patel na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Uledi Mussa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya ambao walitoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini .Kutoka kushoto ni Sheikh Tahir Mahmood Chaundhry, Issa Mwakitalima, Khuram Shahzad na Jamil Mwanga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw. Ian Ferrao (wa pili kushoto) na Meneja Mkuu wa Ushirikiano wa Kampuni hiyo,Bibi. Rosalynn Mworia (wapili kulia) mara baada ya kupokea hundi ya shilingi milioni 100 ikiwa ni mchango kwa waarhirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Ofisini kwake Jana jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Uledi Mussa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa
katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Makundi ya Whats App ya Uongozi na
Leaders Forum, Dkt. Ave Maria Semakafu (wa pili kulia) mara baada ya
kupokea hundi ya Shilingi milioni 16 kutoka kwa wawakilishi hao ukiwa ni
mchango wa makundi hayo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Kutoka
kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Uledi Mussa,Berious Nyasebwa (wapili
kushoto) na Benjamin Thomson wote kutoka Makundi hayo.(Picha zote na Frank Shija, Maelezo)


No comments:
Post a Comment