Mwakilishi wa Timu ya Bongo Fleva, Kalapina (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, wakati makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy na Mwakilishi wa Bongo Movie Steve Nyerere.
Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Bongo Movie Jimmy Mafufu, wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kulia ni mwakilishi wa Bongo Movie Steve Nyerere.
Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Bongo Fleva M2 the P, wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Meneja
Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy
akiwakabidhi vifaa vya michezo wawakilishi wa Bongo Movie na Bongo Fleva kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie
na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la
kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Na Daudi
Manongi, Maelezo
23.09.2016
KAMPUNI ya Tanzania
Sisi Nyumbani (TSN) imejitolea kudhamini pambano la kuchangia wahanga wa
tetemeko la Ardhi Kagera litakalofanyika siku ya Jumapili saa tisa kamili kati
ya Wasanii wa Bongo Movie na Bongo Fleva katika uwanja wa Taifa.
Hayo yamesemwa leo na
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara wa kampuni hiyo Bw.Jahu Mohamed Kessy
wakati akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
“Sisi kama Tanzania
Sisi Nyumbani(TSN) tumejitolea kudhamini pambano hili kwa kushirikiana na
wasanii hawa kwa kuwa tumeguswa na janga hili na hivyo mbali na michango
mbalimbali tukaona ni vyema tujitolee kuwapa Mipila na Jezi kwa wasanii hawa ili kuhamasisha uchangiaji huu ”Aliongeza Bw.Kessy.
Aidha Bwana Kessy
alisema kuwa wao kama TSN wanaunganisha nguvu ya wasanii hawa kutoka katika
tasnia hizi mbili tofauti, kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji huu kwa pamoja.
Pia amewataka
wananchi,mashirika na makampuni mengine binafsi kujitokeza kwa wingi kwa ajili
ya kuchangia na kuwezesha misaada kwa wananchi wa kagera waliopata maafa
kutokana na tetemeko hilo la Ardhi.
Kwa upande wake
mwakilishi wa Bongo Movie Bw.Steve Nyerere amesema kwamba wao kama bongo movie
wameguswa na jambo hili na ndio maana wamejitokeza kutumia vipaji vyao ili kile
kitakachopatikana ili kiweze kusaidia
waathirika wa tetemeko la Ardhi Kagera.






No comments:
Post a Comment