Maafisa wa Serikali ya Tanzania wanasema kuwa watu 11 wamefariki na wengine karibu 200 kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi lililokumba Kaskazini Magharibi mwa Taifa hilo.
Wafanyakazi wa kutoa huduma za misaada wanasema watu kadhaa wamekwama katika vifusi kufuatia kuporomoka kwa mijengo kadhaa.

Inadaiwa kuwa hospitali nyingi katika eneo hilo zimejaa majeruhi.
Mitetemeko hiyo ilihisiwa katika mataifa jirani ya Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Mwandishi wa BBC nchini Tanzania anasema kuwa hilo ndilo tetemeko kubwa zaidi kuwahi kutokea Tanzania kwa zaidi ya mwongo mmoja.


No comments:
Post a Comment