TANGAZO


Sunday, September 18, 2016

TAMASHA LA TIGO FIESTA LAPOKELEWA KWA SHANGWE MKOANI DODOMA IJUMAA HII

Baadhi ya wabunge  wabunge la Tanzania wakiwa wanacheza muziki na msanii Ben Pol kwenyeTamasha la Tigo Fiesta lililofanyika  uwanja wa   Jamhuri   Dodoma usiku wa  kuamkia    jana.
Belle9 akiwapagawisha maelfu ya mashabiki wa muziki waliojitokeza katika viwanja vya jamhuri katika tamasha la Tigo Fiesta.
Jux na Benpol wakiimba wimbo wa pamoja wa NAKUCHANA katika jukwaa la Tigo Fiesta katika viwanja vya Jamhuri mwishoni wa wiki hii.
Wasanii   Bushoke   na Maua Sama   wakifanya shoo ya   pamoja    kwenye   tamasha la Tigo Fiesta usiku  wa kuamkia jana  uwanja  wa   Jamhuri Dodoma.
Christian Bella akitumbuiza mashabiki wa burudani waliohudhuria Tamasha la Tigo Fiesta mapema mwishoni wa wiki hii mkoani Dodoma.
Maua Sama na Nandi wakiimba kwa pamoja katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya Jamuhuri Mkoani Dodoma.
Vanessa na Mcheza shoo wake wakiburudisha maelfu ya wakazi w.a Dodoma waliofika viwanja vya Jamhuri kwenye Tamasha la Tigo Fiesta.
Wabunge wakilisakata Rhumba wakiongozwa  na Msanii Benpol.
Joh Makini na Niki wa Pilli toka Weusi wakilivamia jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika Tamasha la Tigo Fiesta.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson , akifuatilia kwa makini burudani inayotolewa na wasaniii waliopamba jukwaa la Tigo Fiesta  akiwa pamoja na Waziri Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,  Nape Nnauye na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira January Yusuph Makamba) usiku wa kuamkia jana. 

No comments:

Post a Comment