Na Eleuteri Mangi /Beatrice Lyimo, Maelezo, Dodoma.
SPIKA wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amekabidhiwa kitambulisho chake cha Taifa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba leo mjini Dodoma ambacho kinaonesha picha yake, saini yake pamoja na saini ya mtoa kitambulisho.
Hatua hiyo ya Spika Ndugai ya kupokea kitambulisho hicho ni mkakati wa taifa ambao NIDA imekusudia kukamilisha usajili wa vitambulisho vya taifa nchi nzima kwa wananchi, wageni na wakimbizi ifikapo Desemba mwaka huu pamoja na kutoa namba ya utambulisho ambayo itawezesha makundi yote kupatahuduma mbalimbali.
Ili kufikia malengo ya usajili wa ya kusajili Watanzania milioni 24, NIDA imekusudia kutumia taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) milioni 22.7 ambazo watachakatwa na kutoa namba ya utambulisho (NIN) kabla ya kuzalisha kitambulisho cha taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumkabidhi Spika kitambulisho hicho, Waziri Mwigulu alisema kuwa kwa kutumia mfumo wa utambuzi na usajili wa watu utasaidia kuwaunganisha wananchi na mifumo mingine ya huduma ikiwemo mifuko ya hifadhi za jamii, benki, Bodi ya mikopo ya elimu ya juu, RITA na TCRA pamoja na taasisi nyingine zinazotoa huduma.
Awali Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano NIDA Bi. Rose Mdami amemueleza Spika Ndugai kuwa vitambulisho hivyo vinaenda sambamba na mfumo wa utambuzi na usajili wa watu utakaowaunganisha na mifumo mingine muhimu hapa nchini.
Bi. Mdami ameeleza kuwa mfumo huo umeunganishwa na Taasisi muhimu za Serikali ikiwemo TAMISEMI, TRA, TCRA, TASO, NEC, MDA, RITA, Polisi Uhamiaji, HELSB, Mifuko wa Hifadhi ya Jamii ili kuweza kuwa na taarifa za uhakika kwa muhisika.
Amesema kuwa mfumo huo wa utambuzi utaisaidia nchi katika masuala ya usalama, kuweza kuwatambua.


No comments:
Post a Comment