TANGAZO


Saturday, September 17, 2016

SIMBA YAIPIGA AZAM FC BAO 1-0 LIGI KUU YA VODACOM UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

Wachezaji wa Azam FC wakiondoa mpira wa juu uliokuwa umeelekezwa langoni kwao, wakati timu hiyo ilipopambana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo jioni. Katika mchezo huo Simba ilibuka na ushindi wa bao 1-0 na kujinyakulia pointi 3 na kuongoza msimamo wa ligi hiyo baada ya kucheza michezo 4 na kushinda 3 na sare 1.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ibrahim Ajib wa Simba akijaribu kuwatoka mabeki wa Azam FC, Shomari Kapombe (katikati) na David Mwantika, wakati wa mchezo huo.  
Ibrahim Ajib wa Simba akiwa katika harakati ya kuwatoka mabeki wa Azam FC, Shomari Kapombe (katikati aliyefichika) na David Mwantika, wakati wa mchezo huo.  
Ibrahim Ajib wa Simba akijaribu kuwahadaa mabeki wa Azam FC, Shomari Kapombe (katikati) na David Mwantika, wakati wa mchezo huo.  
Ibrahim Ajib wa Simba akiwapenya katikati mabeki wa Azam FC, Shomari Kapombe (katikati) na David Mwantika, wakati wa mchezo huo.  
Laudit Mavugo wa Simba akifuatwa na mabeki wa Azam FC, Shomari Kapombe (kulia) na David Mwantika (kushoto), wakati wa mchezo huo.  
Laudit Mavugo wa Simba akipambana na mabeki wa Azam FC, Shomari Kapombe (kulia) na David Mwantika (kushoto), wakati wa mchezo huo. 
Himid Mao wa Azam FC, akiuondoa mpira wa juu, uliokuwa ukitaka kudhibitiwa na Shiza Kichuya wa Simba.  
Vijana wa Vodacom wakionesha michezo wakati wa mapumziko ya mchezo huo, ambao hadi zinamalizika dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikuwa hazijafungana. 
Wachezaji wa Simba wakiingia uwanjani tayari kwa kukianza kipindi cha pili cha mchezo kati ya timu hizo. 
Mashabiki na wanachama wa Simba wakifuatilia mchezo huo. 
Ibrahim Ajib wa Simba (kushoto), akiwania mpira na Bruce Kangwa wa Azam FC.
Shiza Kichuya wa Simba akishangilia bao pekee katika mchezo huo, aliloifungia timu yake hiyo.
Wachezaji Mzamiru Yassin (kushoto) na Laudit Mavugo (kulia) wote wa Simba, wakishangilia bao hilo lililofungwa na Shiza Kichuya mbele ya picha ya aliyekuwa mchezaji nyota wa timu hiyo, Mafisango, ambaye alishafariki. 
Laudit Mavugo akiwa amembeba mchezaji Shiza Kichuya baada ya kuipatia timu yao hiyo bao pekee na la ushindi katika mchezo huo. 
Mashabiki wa Simba wakishangilia bao hilo. 
Ibrahim Ajib (katikati) wa Simba akiwa amezongwa na mabeki wa timu ya Azam wakati akijaribu kuwatoka kuelekea kwenye lango la timu hiyo.

No comments:

Post a Comment