Watanzania wakiishangilia timu yao ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (U17), Serengeti Boy, wakati ilipokuwa ikipambana na wenzao wa Congo Brazzavile kuwania kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya miaka 17 mashindano yatakayofanyika nchini Madagascar 2017. Serengeti Boys wameshinda kwa mabao 3-2, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Hapa ubao wa matangazo ukionesha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (U17), Serengeti Boy, ikiwa imeshinda bao 1-0 katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hapa ubao wa matangazo ukionesha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (U17), Serengeti Boy, ikiwa inaendelea kuongoza kwa kupachika mabao 2-0 katika kipindi hicho hicho cha kwanza cha mchezo huo.
Watanzania wakishangilia bao la pili la timu yao ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (U17), Serengeti Boy dhidi ya Congo Brazzavile katika kuwania kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya miaka 17 mashindano yatakayofanyika nchini Madagascar 2017.
Watanzania wakishangilia kwa nguvu timu yao ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (U17), Serengeti Boy baada ya kuifunga Congo Brazzavile bao la pili.
Wachezaji wakishangilia bao hilo la pili dhidi ya Congo Brazzavile Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Serengeti Boy ilikuwa ikiongoza kwa mabao hayo kama ubao wa matangazo unavyoonesha dhidi ya Congo Brazzavile katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya miaka 17 mashindano yatakayofanyika nchini Madagascar 2017.
Mchezaji Mohamed Rashid akimtoka Ngumbi Exau wa Congo Brazzavile.
Hapa Mohamed Rashid akimwacha Ngumbi Exau wa Congo Brazzavile.
Issa Abdi wa Serengeti Boys akimtoka Mantourari Aldo wa Congo.
Issa Abdi wa Serengeti Boys akiwania mpira na Mantourari Aldo wa Congo.
Mpigapicha wa Azam Tv akiwa kazini wakati wa mchezo huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akishangilia pamoja na wananchi wakati wa mchezo huo.
Watanzania wakishangilia timu yao ya Serengeti Boys.
Muhsini Malima wa Serengeti Boys akitafuta mbinu ya kumtoka Moundza Prince wa Congo.
Hapa ubao wa matangazo ukionesha Tanzania mabao 2 na Congo 1, baada ya timu hiyo kujipatia bao moja kwa njia ya penalti baada ya mchezaji wao kudondoshwa kwenye boksi la 18.
Hapa wachezaji wa Serengeti Boys wakishangilia bao la 3 baada ya kuwachukua dakika chache tu baada ya kufungwa bao hilo la penalti na Congo.
Hapa wachezaji wakishangilia bao hilo.
Ubao wa matangazo ukiuonesha Tanzania mabao 3 na Congo bao 1.
Hapa Congo wakiwa wameongeza bao la pili na kuufanya mchezo huo kuwa Serengeti Boys mabao 3 na Congo mabao 2 mpaka mwisho wa mchezo huo.
Hapa mchezo ukiwa umemalizika na vijana wa Serengeti wakitoka nje ya uwanja na ushindi wa mabao 3-2.
Hapa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Hapa wachezaji wa Congo Brazzavile wakiondoka uwanjani pamoja na viongozi wao baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

No comments:
Post a Comment